Jumatatu, 25 Agosti 2014

KARIBU KATIKA SOMO LA VITA VYA KIROHO.2KORINTHO 10:3-5.EFESO 6:12.

Dibaji:Kama waamini tunaitaji kujua kuwa tunavita, katika ulimwengu huu tunaoishi kuna aina mbili ya falme kuna ufalme wa giza na ufalme wa nuru.Ufalme wa giza unatawaliwa na shetani na mapepo yake na ufalme wa nuru unatawaliwa na Yesu Kristo.Kwahiyo vita hii inahusisha watu waliyoko chini ya ufalme wa Mungu dhidi ya ufalme wa giza.Unapomkubali Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wako moja kwa moja unakuwa adui wa ufalme wa shetani.Sasa kama waamini tunahitaji kujifunza namna gani tunaweza kukabiliana na vita hivi!Lazima tujue tunayomamlaka  juu ya shetani na majeshi yake.Vita hivi ni vya kiroho sio vya kimwili.Uwanja  mkubwa wa mapambano ni kwenye  mawazo au akili zetu.Shetani hupandikiza mawazo mabaya  ndani yetu,yanayopingana na Neno la Mungu na mapenzi ya Mungu.

A.MUUNDO WA UTAWALA SHETANI  WA SHETANI:WAEFESO 6:10-13.
1.Shetani.
Shetani ni mkuu wa utawala wa giza Biblia ina mwita mfalme wa uwezo waanga.Efeso 2:2.
2.Falme.
Falme ni mashetani wa wakilishi wa utawala wa shteni wanaotawala falme kubwa,kimfano mabara kama vile africa,africa mashariki, ulaya ,asia na nk.
3.Wenyemamlaka.
Wenyemamlaka ni mashetani yanayotawala nchi,kupitia tawala za wanadamu.
4.Wakuu wa giza.
Nimashetani yanayotawala manbo ya giza ya kishetani kimfano,uendelezwaji wa dhambi,umaskini,ujinga na magonjwa.
5.Majeshi ya pepo wabaya.
Yanaitwa majeshi kwasababu yapo mengi na yote hayana kazi moja yanafanya kazi kama vikosi vikosi.Kama vile katika mataifa yetu tunamajeshi yaliyogawanyika katika utendaji tofauti tofauti.
6.Binadamu wanaomtumikia  shetani walioingia mkataba au agano na shetani ili kumtumikia.Kama vile wachawi,maajenti nk.

B.SILAHA ZETU ZA KUJIHAMI{KUJILINDA}EFESO 6:10-18.
1.Chepeo ya wokovu{kofia}kolosai 1:13.
Chepeo ilikuwa silaha yaani kofia ya chuma iliyovaliwa na askari wa kirumi kuhifadhi kichwa na mashambulizi ya adui.Kiroho chepeo ya wokovu,hulinda akili zetu kutokana na mashambulizi ya shetani.{Kujua ukombozi wako katika Kristo ni ulinzi}
2.Dirii ya haki kifuani.
Dirii ya haki ili kuwani ni fulana ambazo risasi haiwezi kupenya.{bullet proof vest}
Waamini ambao hawajapata ufahamu wa haki ya Kristo wameacha roho zao wazi kwa ajili ya kushindwa.
Tumepewa haki ya Yesu kama zawadi sio kwa kustahili kwetu bali kwa neema yake tu.
Sasa tunao wajibu wa kuishi katika haki kwa kutii neno la Mungu.2Kor.5:21.Nikama mfano raia wa nchi 
asiyejua haki zake kama raia nilahisi kupoteza hazako za msingi.Mafundisho mengi leo kuhusu kuvunjiwa laana na kufanyiwa maombi ya ukombozi,mengi ya hayo yamejengwa katika msingi wakutokujua haki zetu ndani ya Kristo kupitia msalaba wake.
3.Kweli viunoni.
Huu ulikuwa ni aina ya mkanda ulifungwa kiunoni,kumsaidia askari mavazi yake kushikamanishwa vizuri na mwili wake na kutokupata shida awapo vitani.Kiroho kweli hii ni tabia  ya Mungu ambayo kwa mwamini hufanyika silaha ya kujilinda.Kwasababu adui hana hiyo kweli.Tabia hii inampa mwamini ujasiri wa kukabiliana na kila changamoto katika maisha yake ya imani.
4.Utayari wa injili ya amani.
Utayari wa kutumika  hiyo ni silaha kali dhidi ya adui.2Tim 4:2.Unapokuwa unasukumwa sukumwa ili kumtumikia Mungu ujue unapoteza silaha yako dhidi ya adui.Kumbuka shetani na majeshi yake wanafanya kazi kwa bidii usiku na mchana,hapotesi kila fursa inayotokea mbele yake.
5.Ngao ya imani.
Askari wa wakati ule alitumia ngao iliyokuwa ngozi ya mnyama ilitengenezwa kwa mfano wa kama vile ungo ili kuzuia mishale yenye moto isimdhuru mpiganaji.
Imani hufanyika kama uzio wetu wa ulinzi ili kuzima mishale yenye moto.
C.SILAHA ZETU ZA KUSHAMBULIA.
1.Upanga wa Roho{Neno la Mungu}
Tunaweza kufanya kufanya mashambulizi kwa kutumia Neno la Mungu.Ufu.1:16;2:16.Ebr.4:12.Kwa maana hii sasa tunahitaji kulihamisha Neno la Mungu katika kurasa za Biblia na kuliweka ndani ya mioyo yetu,linapotoka ndani ya mioyo yetu kupitia vinywa vyetu huitwa upanga wa Roho.Hii ndiyo silaha ambayo Yesu alitumia ili kumshambulia shetani na hatimaye kumshinda.Math.4:4-11.
2.Jina la Yesu.
Unapompokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wako unapewa haki ya uwakili wa kutumia Jina la Yesu.Yoh.16:23-24,Uf.19:13.Kwa kutamka Jina la Yesu unaweza kuharibu kazi zote za shetani.
3.Imani ni silaha ya kujilinda na kushambulia.1Yoh.5:4.Imani ni njia Yetu ya ushindi dhidi ya ya ulimwengu.
4.Kuomba katika roho yaani kunena kwa lugha ni silaha yenye nguvu.
 -Ina mjenga mwamini na kumwimalisha
 -Maana ya kujenga ni kuinua,kufanya jasiri,kutia nguvu mpya.1Kor.14:4.
5.Sifa.
Sifa ni silaha yenye nguvu dhidi ya adui.
 -Sifa humtukuza Mungu
 -Sifa humsimamisha na kumzima shetani.Zab.8 na 9.
D.MADHAIFU YA SHETANI.
 Ufunguo kwa ushindi katika.
Kujua udhaifu wa adui yako,unakuwa na asilimia kubwa ya kushinda.Shetani huwa anatusoma maeneo yetu ya udhaifu na kushambulia hayo maeneo.
1.Hawezi kutenda kazi katikati ya sifa.Zab.22:3.
Sifa humsimamisha na kumnyamazisha adui.Huteka na kuzishinda ngazi zote za majeshi ya adui.
2.Hawezi kutenda kazi wakati Neno la Mungu limenenwa.Uf.1:16.
3.Hawezi kufanya kazi katika Jina la Yesu kwa sababu limeinuliwa juu ya majina yote.Flp.2:8-11.
4.Hawezi kufanya kazi katika upendo kwa sababu yeye asili yake ni chuki.1Kor.13:13.
5.Hawezikunya kazi katika nuru.Kwasababu yeye ni giza.Zab.119:105.
 -Neno liingiapo,huleta nuru au mwangaza.Zab.119:130.
 -Unaposimamia  Neno la Mungu ni sawa na kama umewasha mwangwa wa taa makali.
6.Hawezi kufanya kazi mahali penye kweli.Neno ndiyo kweli.Yoh.17:17,8:44.
7.Hawezi kufanya kazi wakati Neno la Mungu limepewa mamlaka ya kwanza na ya mwisho katika maisha yako.Yoh.6:68.



















Ijumaa, 22 Agosti 2014

KARIBU KATIKA SOMO LA UANAFUNZI KAMA YESU ALIVYOFUNDISHA.MATHAYO 28:18-20.

Dibaji:Shauku ya Yesu nikuona kuwa wanapatikana wanafunzi katika mataifa yote.Katika lugha ya kiyunani Neno  enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi imeelezewa yaani ni kila kundi la kabila hapa duniani.Wajibu wetu ni kuwafanya watu kuwawanafunzi wanatii Neno la Mungu.
Mafanikio katika huduma hayapo katika wingi wa watu tulionao.Swali ni kwamba wangapi tumewaongoza kuwa wanafunzi wa Yesu?
Kinyume chake ni kushindwa,matokeo yake ni kuwa na mbuzi wengi kuliko kondoo.Mathayo 25:31-46.

YESU ANAFAFANUA UANAFUNZI: Yoh.8:31-32.
Uanafunzi ni hatua ya kwanza katika mahusiano na Mungu.Ina maana ni watu waliokubali kutubu dhambi zao na kumkubali Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao na kuwa tayari kutii Neno lake.
Wanafunzi wa kweli ni wale wanaokuwa tayari kudumu katika Neno lake.
Neno la kiyunani la mwanafunzi ni Mathetes-Linapatika mara 261 katika agano jipya.
Ambapo neno Mwamini  kiyunani Postos-Linapatika mara 9 katika agano jipya.Neno Mkristo kiyunani hupatika mara 3.
Kwa msingi huu sasa tunaweza kuhitimisha kuwa wale waliomwamini Bwana mwanzoni waliitwa wanafunzi.

VIGEZO VYA YESU JUU YA MWANAFUNZI.
1.Kuzaa matunda.Yoh.15:8-36.Tunapozaa matunda hilo huthibitisha kuwa sisi ni wanafunzi wa Yesu.Yapo matunda ya aina nyingi tunayopaswa kuzaa ila baadhi yake ni Tunda la Roho Mtakatifu tazama Gal.5:22-23.Tunda hili hufunua tabia ya Yesu katika maisha ya mwamini.Kwasababu hiyo ndilolinaleta tofauti kati yetu na wale ambao hawajaokoka.Mwamini anapozaa tunda la dhambi hiyo ni alama ya wazi kuwa hataokoka.Gal.5:19-21.Kuna matunda kama utumishi wetu kwa Bwana kuwaleta watu kwa Kristo na nk.Yoh.4:34-39.
2.Kuumpa Yesu nafasi ya kwanza katika ya mtu.Luka 14:25-26.Yoh.12:25.
Yesu hakulidhika na makutano mengi waliokuwa wakimfuata hakuwa kafikia lengo lake.Yesu anatafuta watu watakaompenda Mungu kwa mioyo yao yote akili,nafsi na nguvu zao,yaani wanafunzi.
Yesu hakuwa na maana ya kuwachukia wazazi wetu na ndugun zetu.Hii ni lugha ya kimfano,Yaani kama unataka kuwa mwanafunzi lazima tumpende yeye kuliko vyote.Mwanafunzi hutii na kushika amri zake yesu.Yoh.14:21.
3.Mtu yeyote asiyechukua msalaba wake.LukA 14:27.
Hapa pia anatumia lugha ya kimfano;kawaida ya warumi waliwasulubisha wahalifu kwenye kwenye njia kuu nje ya malango ya mji ili watu wengine waogope kufanya uhalifu."Beba msalaba wako"Msemo huu ulikuwa wakaida nyakati za Yesu.
Wahalifu waliogopa kusikia maneno  hayo,walijua ndiyo mwanzo wa saa ya mateso makali sana.
Msemo huu ulimaanisha =Kukabiliana na mateso magumu yanayokwijia ambayo hayaepukiki.
Mwanafunzi wa kweli yupo tayari kuteseka kwa ajili ya kumfuta Yesu.Flp.1:29.
Atakuwa tayari kuhesabu gharama.Luka 14:28,32.
Alichomaanisha Yesu ukitaka kuwa mwanafunzi wake,hesabu gharama mapema,ili usije ukakata tamaa mambao yatakapokuwa magumu.
4.Asiyeacha vyote alivyonavyo.Luka 14:33.Hii ni kauli ya kimfano;hakuwa na maana ya kuacha vyote tulivyonavyo tutaishije?Nilazima tuachilie kila kitu tulichonacho kwa maana ya kumkabidhi Mungu avimiliki na kufikia kiwango cha kutokutumikia mali,bali kumtumikia Mungu kwa mali zetu.
Kabla ya kufikiri kufanya wengine kuwa wanafunzi tunapaswa sisi wenyewe tuwe na hakika kuwa sisi ni wanafunzi.
















Jumanne, 19 Agosti 2014

KARIBU KATIKA SOMO LA KANUNI ZA IMANI ZILETAZO MATOKEO.ZABURI 89:34;MALAKI 3:6.

Dibaji:Mungu aliwambia Israeli MIMI NI MUNGU NISIYEBADIRIKA.Neno la Mungu huwa halibadiriki ili kuendandana na mazingira.Inamaana mazingira yeyote hatakama nimagumu yakiwa nje ya uwezo wetu kama wanadamu bado hayawezi kulibadiri Neno la Mungu.
Mungu huwa habadiriki ila yeye huwa ana sifa ya kubadilisha.Mungu hadhuriki na chochote kinachoendelea Ulimwenguni huu.
Unaweza kumtegemea Mungu ambaye akisema amesema yeye huwabadilishi kauli yake.Nitofauti na wanadamu ambao leo wanaweza kusema bila kutekeleza walichosema.
Kwakutambua kanuni hizi humfanya mwamini awe na imani isiyoyumba katika Mungu wake.Kwasababu hiyo hupokea mahitaji yake.
A.TAFUTA AHADI KATIKA NENO LA MUNGU KWA KILE UNACHOHITAJI.
Mungu wetu anaishi ndani ya Neno lake na anatenda kazi kwa msingi wa Neno,hakuna njia ya kukutana na Mungu ila ni kwa msingi wa Neno lake.
Kunambo mawili amambayo kamwe hayawezi kubadilishwa au kubadirika.WABRANIA 6:13-18.ZABURI 138:2.
 1.Ahadi za Mungu
 2.Kiapo cha Mungu
-SHIDA YA WAKRISTO WENGI NI KWAMBA:
 1.Hawazijui hizo ahadi
 2.Hawaamini hata wanapozijua
 3.Wanakaza macho sana  kwa shetani na yale anayosema

B.LIAMINI NENO LA MUNGU.
TITO 1:2;HESABU 23:19.Kwasababu Mungu hawezi kusema uongo,anachosema kwako atafanya.
Nilini na kwa namna gani hilo huwajibikinalo.Wewe unawajibika na kumwamini,kuwa hawezi kusema uongo.
1.Wewe unawajibika alichosema nini kisha..
2.Uwe na uhakika wa ndani  kabisa kuwa hawezi kudanganya.Mashaka ni kikwazo kikubwa cha kupokea kutoka kwa Mungu.Mk.9:23.

C.USIFIKIRI HALI ZINAZOONEKANA KUPINGANA.IIKor.4:18.
Yakitambo=ya muda tu yaani siyoyakudumu.Kwa lugha nyingine mambo yenyeuwezekano wa kubadirika.Chochote unachokiona kwa macho yako hicho si chakudumu,kipo katika hali ya kubadirika.
Badilisha mtazamo wako juu ya matatizo,majaribu ya napokuja Mungu pia huja kwa msaada wake.
Mf.Lk.8:41-50.Ukisoma Maandiko haya utaona hapa kuwa mazingira yaliyopingana kabisa, lakini bado Mungu alifanya muujiza.
Angalia jawabu la tatizo badala ya kutafakari tatizo lenyewe.IIFalm 6:8-16.
Lione Neno kama linakidhi kikamilifu kukuvusha kwenye tatizo hilo.
1.Ulitambue tatizo
2.Usitafakari wala usiendelee kuliangalia
3.Usiendelee kulizungumuzia.Kuna baadhi ya watu hata wakisha mwomba Mungu bado wanakuwa wakizungumuzia tatizo hilo kila wanapokwenda.
4.Nenda kwenye Neno la Mungu ambalo imani yako hutokea.
5.Jibu hilotatizo ukisimama katika Neno la Mungu.Mk.11:23.Mlima utaondoka kwa kuumbia sio kwa kuutazama tu na kusikitika.
6.Ona yasiyoonekana kwa jicho la IMANI.Imani ni jicho la imani kuona yale yasiyoonekena kwa macho ya kimwili.
D.MSIFU MUNGU KWA AJILI YA JIBU.ZAB.119:89.ZAB.150:1.
Imba kwa imani msifu Mungu kwa jibu hata kama hujaliona kwa macho ya kimwili.
























Jumamosi, 16 Agosti 2014

KARIBU KATIKA SOMO LA MOYO ULIOTHABITI.ZABURI 112:7-8;125:1.

Dibaji.Zaburi  hii ni maelezo ya mtu ambaye moyo wake uimara katika Neno la Mungu.Hayumbishi na habari mbaya,moyo wake umethibitika ukimtumaini Bwana.Misingi huu unakupa ujasiri wa kukabiliana na yasiyotarajiwa katika maisha.Kukosa moyo thabiti katika Neno la Mungu ndipo unasikia leo watu wamekunywa sumu au kajinyonga ukichunguza chanzo cha matukio haya ni changamoto katika maisha.Kupitia somo hili tutakwenda kujifunza mambo ya msingi yanayoweza kuwa msaada mkubwa katika maisha yetu.
A.KUTAMBUA NYAKATI TUNAZOISHI LEO:
Nyaki hizi zinatoa mwangwa mkubwa kwa masumbufu,kuogopa,kutishwa kwa urahisi na habari mbaya.Mahali dhambi ilipo na neema inakuwepo kwa wingi.RUMI.5:20.
1.Mwamini anawezaje kuishi katika nyakati hizi?Anaweza kuishi moyo wake ukiwa imara ukimtumaini Bwana,pasipo kuogopa chochote kinachotokea duniani leo.Zab.112:8.
2.Kufikia kiwango cha mzaburi huyu.
Fika mahali pakutoenda kwa msukumo wowote,sikwa yale unayosikia au kuona.Moyo uliothabiti unajua kuwa Mungu anatosha na kuzidi naye atakutana na kila hitaji letu.Filp.4:19.

B.MOYO ULIOTHABITI UNAMTUMAINI BWANA.
Kama unatarajia kumtumaini Bwana lazima uamini Neno.Neno na Mungu ni kitu kimoja.RUMI.12:2;1Yoh.1:1.
1.Ishara za kurudi kwa Yesu na mwisho wa dunia.Math.24.Yesu alikuwa akifundisha kuhusu ishara za kurudi kwake hakusema siku au mwezi,mwaka nk.Yeye alitoa maelezo yanayohusu ishara zitakazo onyesha dalili za kurudi kwake na mwisho wa dunia.Yesu alifundisha  katikati ya mashambulizi ya shetani hatupaswi kusumbuka,tunapaswa kuishi juu ya viwango vya dunia.
2.Mtu asiwadanganye.Math.24:4.
Yesu alitambua  katikati ya hizo ishara za kurudi kwake,kutakuwa na mabomengi,yatakayo hubiriwa ambayo ambayo sio injili halisi.Mafundisho na mahubiri leo ni baraka yaani mafanikio ya kimwili tu.Yesu anakuwa kama mganga wa kienyeji anayefuatwa kwa lengo la kuwapa watu mafanikio kisha wafe waende motoni.Injili kuhusu toba,utakatifu ,wokovu imekuwa adimu kusikia.watu wanajua aina za baraka kuliko wanavyomjua mtoa baraka hizo.Kabla ya kuwahubiri watu baraka na mafanikio kwanza tuwahubiri mambo ya msingi kuhusu ufalme wa Mungu.
Niwajibu wa mwamini kutofautisha kati ya ukweli wa injili na mafundisho ya uongo.Mdo17:10-11.
3.Habari ya vita na matetesi ya vita{msitiswe}Math.42:6.
Lazima kutakuwa na njia ya kwetu ya kuishi katikati ya machafuko hayo.
4.Habari njema itahubiriwa.Math.24:14.Katikati ya habari mbaya na ngumu,kutakuwepo na mtu atakayesimama na kuhubiri habari njema.Ipo njia ya kuishi hapa duniani katika wakati huu pasipo kuogopa au kutupwa huko na huko na kila matatizo unayokutananayo.
Unaweza kujaa Neno la Mungu na kuwa imara.
C.MIFANO YA WATU WALIOKUWA NA MOYO THABITI.
1.Mtume Paulo.Rumi.8:31-39.Unaposoma mistari hii utaona ukiri wa mtu ambaye moyo wake ni thabiti katika Neno la Mungu.Wakati huu Paulo alikuwa anapitia kipindi kigumu cha vita bado alikuwa thabiti hakuona kitu cha kumtenga na upendo wa Mungu.Mapito ya Mtume Paulo.IIKor.11:22-32.
2.Mjenzi mwenye akili.Math.7:24-27.Anaelezea watu wa wili waliosikia Neno,mmoja alisikia na kutendea kazi Neno akawa imara katika Neno.Mwamba ni Neno.
Wapili alikia lakini hakutendea kazi Neno,akawa hana msingi,kwasabu hiyo hakuweza kuhimili dhoruba na mafuriko ya maisha.
Shetani atakuwa kwa urahisi ujenge msingi wa Neno la Mungu katika maisha yako.Ndiyo maana leo kunavita na ushindani mkubwa kwa waru kwenda kanisani na kujifun za Neno la Mungu,baadhi ya watu wanasoma Biblia jumapili kanisani,nyumbani akisoma anasinzia na kulala,watu wengi leo hawapendi kujifunza siri za mbinguni kupitia mafundisho ya Bilblia,wengi wanasinzia hadi katika ibada kanakwamba haikutosha walivyo lala vitandani mwao!kwenye biashara na maofini hawalali wala kusinzia hii ni ajabu.
Shetani atafanya kila awezalo kukuzuia kusonga mbele katika imani,ila kwa msaada wa Bwana tutashinda.Filp.4:13.
3.Yairo mkuu wa sinsgogi.Lk.8:40-42.Yairo aliamini moyoni mwake kwa Yesu kuweka mikono yake juu ya binti yake kuwa atapona na kuishi.Mk.5:12-35.Wakienda kwake mawanamke mwenyekutokwa na damu alikamatamwelekeo wa Yesu.Wakati Yesu akimuhudumia,wajumbe wakaja na kumweleza Yairo binti yako amakufa,kwa nini uendelee kumsumbua mwalimu?Hili lilikuwa kama shinikizo la shetani,Yairo akili kushindwa na kumlalamikia Yesu na yule mwanamke.
Katika mazingira kama haya wengi wamepoteza baraka za Mungu.Mk.11:24.Imani inasema ni vyangu sasa ,mazingira yanapinga kuwa huwezi kupokea.Kuna mazingira unaweza kusema Neno au kukaa kimya.Yesu hakusitushwa na habari ya wale wajumbe wa kushangaa.Jibu la Yesu usiogope amaini tu,mst.36.Mariko.Yesu anamtia moyo awe kama mzaburi wa Zabu.112.Asiyeogopa habari mbaya.Baada ya wajumbe kuja na habari  mbaya kjwa kweli mazingira yalionekana kushindikana kabisa.Kutokushituliwa na habari mbaya  huo ndiyo ulikuwa msingi na mwenendo wa maisha ya Yesu hapa duniani.
Matokeo yake binti alifufuka,moyo wake ulikuwa umethibitika kwa kile alichoamini.
4.Sababu ya wa kristo kunyan'ganywa baraka zao.
Nikwa sababu ya kushindwa kuliingiza Neno la Mungu katika mioyo yao na mioyo yao kuwa thabiti.
Mkristo mnyonge na dhaifu ni yule ambaye haelewi agano lake na Mungu.
Ikiwa utaripa Neno la Mnngu nafasi ya kwanza katika maisha yako na kuliweka juu ya vitu vyote,litaumba sura ya Yesu  katika maisha yako au katika moyo wako.Utaona matokeo yale yale aliyoona Yesu akiwa hapa duniani.
Yesu hakuwahi kushindwa.Mwamini amevikwa vitu vile vile alivyokuwanavyo Yesu hapa duniani.Yaani Neno la Mungu lenye mamlaka yote.

















M



Alhamisi, 14 Agosti 2014

KARIBU KATIKA KATIKA SOMO LA UTHAMANI WA NENO LA MUNGU.IITIMOTHEO 3:16-17.YOHANA 6:63.

Dibaji:Mafundisho ya msingi lazima ya jengwe katika maisha ya mwamini hili litampa mwamini nguvu ya ushindi.Kutoelewa uthamani wa Neno la Mungu,hatimaye nikuwa na maisha duni ya kiroho.
Nivingumu kuthamini kitu usichojua uthamani wake.
Williamson alitemblea mwanduwi Shinyanga akawakuta wazee wa kisukuma wakicheza bao kwa kutumia vipande vya arimas,bila kujua wanachezea utajiri.Williamson akawazidi mahesabu hawa wazee ni kwasababu yeye alijua uthamani wa madini ya arimas.Alienda kuwanunulia groli za mvilingo zenye rangi ndani akawaomba,waupe hayo mawe ili awape groli mbazo ni nzuri zaidi kwa kuchezea bao.Wakampa bule akaenda kuuza uraya na kurudi na fedha nyingi na kununua eneo ambalo mpaka leo kuna  machimbo ya madini.Huu ni mfano  mzuri kwa wakristo wasiojua uthamani wa Neno hawana tofauti na wale wazee wa kisukuma.
 Sasa twendwe kuchunguza kwa makini juu ya uthamani wa Neno la Mungu.
1.Neno la Mungu.Yoh.1:1.Maneno ya mtu hufunua moyo wake na mawazo yake.Kriso kama Neno alifunua,moyo na mawazo ya Mungu.Ebr.1:1-2.
Mungu leo anasema nasi kupitia Neno lake.
2.Neno linashikilia Uumbaji.Ebr.1:3;Mwa.1:1.Ebr.11:3.
3.Neno ni chakula cha mtu wa ndani.Yaani roho yako.roho yako inahitaji chakula cha Neno,kama mwili wako unavyohitaji chakula cha kawaida.Math.4:4;Ayu.23:12;Yer.15:16.
4.Kwa Neno tunazaliwa upya.Mwanadamu huwa anazaliwa mara mbili mara ya kwanza kupitia mahusiani ya wazazi wetu, mara ya pili ni kupitia Neno la Mungu.Efe.2:10,Ipet.1:23;Yak.1:18.IIKor.5:17.
5.Neno ni upanga wa Roho.Efe.6:17.Neno ni moja ya silaha yetu ya kushambulia adui.Kwa luhga nyingine ni silaha dhidi ya shetani.Uf.2:16;1:16;Math.4:4;7;10.
6.Neno linaponya.(nidawa)Tunaposimama katika Neno la Mungu tunapokea kile ambacho ni haki yetu.Mith.3:8;4:22,Zab.107:20,Math.8:8,13.Math.8:16.
7.Neno linatupa maisha malefu.Mith.3:2;4:10;22;9:11.Mungu alikusudia tuishi kulingana na Neno lake,nje ya Neno maisha yetu yanaweza kufupishwa na maisha ya dhambi.
8.Neno linatupa amani.Meth.3:2;Zab.120:165.
9.Neno linatupa hekima.Mtu aliyejaa Neno la Mungu  ni mtu amabae hekima ya Mungu inaweza kuoneka kupitia yeye.Mith.2:1-6.
10.Neno litatupa ulinzi.Kupitia Neno tunakuwa salama.Zab.119:9.
11.Neno linatupa ushindi dhidi ya dhambi.Moyo usio na Neno ni kama nyumba isiyo na milango inakuwa haipo salama.Zab.119:9.
12.Neno linatupa mafanikio.Mungu anapo tubariki na kutuinua hayo yote huyafanya kwa msingi wa Neno lake,yeye hutenda kazi kwa msingi wa Neno.Yos.1:8;Zab.1:2-3.Math.7:24-27.
+Mambo ya kufanya katika kitabu cha torati.
   -Kisiondoke vinywani mwetu
   -Tutafakari maneno yake mchana na usiku.
   -Tupate kutenda sawasawa na yaliyoandikwa humo.Math.25:31-46.
Matokeo yake ni kustawi kiroho na kimwili.
13.Neno linatufanya kuwa washirika wa tabia ya kiungu.IIPet.1:4.
14.Neno linatupa kila kinachotuongoza katika uzima na utauwa.IIPet.1:3.
15.Neno ni chanzo cha imani yetu.Imani yetu inachanzo katika Neno la Mungu,na inastawishwa na Neno la Mungu.

















Jumanne, 12 Agosti 2014

KARIBU KATIKA SOMO LA KUGUNDUA KUSUDI LA MUNGU KWA KIJANA.KUTOKA 2:1-4.WAEBRANIA 11:24.

Dibaji.Upo umuhimu wa kugundua kusudi la Mungu katika maisha yako kama kijana,kwa sababu haupo duniani kwa bahati mbaya wewe sibahati mbaya hata kama wazazi wanaweza kusema walikuzaa kwa bahati mbaya,wao wanaweza kuona hivyo kwa sababu ya ufahamu wao wenye mipaka.Ila kwa Mungu sibahati mbaya.Mungu hanaga bahati mbaya wewe ni kusudi la Mungu wewe ni mpango wa Mungu,wewe ni ndoto ya Mungu.
Musa alizaliwa katika nchi ya Misri wakati wazazi wake wakiwa utumwani,kipindi alichozaliwa alikuta sheria imeshapitishwa kuuwawa kwa watoto wote wa kiume wanaozaliwa katika nchi ya Misri.Kwasababu yeye hakuzaliwa kwa bahati mbaya kama wewe msomaji wangu hakufa kwa sheria ya mfalme matokeo yake alikwenda kuishi katika nyumba ya mfalme yaliyetoa amri hiyo na kumlea kama mtoto wake.Akiandaliwa kuwa mfalme wa Misri,pamoja na yote aliyotendewa bado alijua kuwa yeye hakuwa mtoto wa Farao,kwa sababu alihitaji kusimama katika kusudi la Mungu.
Kutokugundua sababu ya kuwepo kwako duniani,utajikuta unaishi katika maisha ambayo ni kama mashua iliyo bahari isiyokuwa na mwelekeo.
Matokeo yake ni kutekwa na desturi mbaya za maisha ya dhambi.Kama vile ulevi,uzinzi,madawa ya kulevya,ujambazi nk.

  • Ni muhimu kujiuliza maswali haya:

         Je,wewe ni nani?
         Ndoto zako nini katika maisha?
         Una umuhimu gani kwa Baba yako na Mama yako,ndugu zako Taifa lako, kijiji chako?
         Wajibu wako katika jamii ni upi?
         Matarajio na malengo yako katika jamii ni yapi?
        Jamii yako inatarajia nini kutoka kwako?
        Je,mambo gani yanayodumisha ukamilifu wako,kimwili,kijamii,kisaikolojia,kiuchumi na kiroho?.

TUNAKWENDA KUJIFUNZA  SABABU TANO ZA KUWEPO KWAKO HAPA DUNIANI:
 Kila mwadamu mwenye akili timamu anahitaji kujitambua,kuna umuhimu mkubwa sana katika              kujitambu.Kama hujitambui huwezi kulinda uthamani wako.

1.UMEUMBWA ILI KUMPENDEZA MUNGU.KOLOSAI 1:16.

Lazima utambue kuwa umeubwa kwa ajili yake,Mungu.Wajibu wako ni  kumpenda Mungu.Kumpenda Mungu nikupenda anachopenda na kuchukia anachochukia.Mwaanzo 39:9.
Kwasabubu hiyo kila kitu kinachokuhusu kinapaswa kuanza na Mungu na kuishia na Mungu.
Hili hudhihilishwa na kumwabudu Mungu na kuwa na ushirikiano naye.Huu ndiyo wito wetu  mkuu.KUTOKA 3:12.Kama huwezi kumwabudu Mungu pia huwezi kumpendeza na hata kumtumikia.Yoh.4:23-24.Math.4:8-10.
Kuabudu ni zaidi ya kwenda jumapili kanisani,kunahusu mfumo mzima wa maisha yetu kaika kuishi kama atakavyo yeye.

2.UMEUMBWA ILI UWESEHEMU YA FAMILIA YA MUNGU.YOHANA 1:12.

Naweza kusema kuwa hapa duniani kuna makundi mawili ya watu,watoto wa Mungu na watu wa Mungu.Ebr.2:10,Yoh.1:12.Ili kuwa mtoto wa Mungu ni pale unapo mkubali Kristo kuwa Bwana na Mwokozi katika maisha.Kinyume chake utabaki kuwa mtu wa Mungu.Mpango wa Mungu wa kuwa na familia ulikuwepo kabla ujazaliwa.
Huwezi kuwa nje ya Yesu na bado ukawa sehemu ya familia ya Mungu.Kanisa hatujiungi kama klabu bali kwa kuzaliwa upya.Yoh.3:3.
Biblia inafunua wazi kuwa kunafamilia mbili ya shetani na ya Mungu.Yoh.8:44.Umepewa uamuzi wa kuchugua kuwa familia ya Mungu au ya shetani.

3.UMEUBWA ILI UFANANE NA KRISTO.WARUMI 8:29.

   Kusudi kuu la wokovu ni kutuleta katika  kufanana Kristo.Kwa maana ya Kristo kuonekana katika        maisha yetu.IKor.11:1.
                         
          Ni nini maana ya kufanana na Kristo? I Yoh.2:6. 

  • Kufanana na Kristo ni kumpenda Mungu na kuwapenda watu wengine.Math.22:37;IYoh.4:20-21.Upendo wa Mungu kwa waamini hutuchochea kuwapenda watu wengine.
  • Pendo hudai uaminifu wetu kwa Mungu.Ebr.3:2.

           Tunamwona Yesu akiwa tayari kuyatimiza mapenzi ya Mungu kwa kutoa maisha yake kwa                    ukombozi wetu.Math.26:42.Tunapaswa kuwa waaminifu kutimiza mapenzi yake bila kujari                  ghalama.

  • Pendo la Kristo lilifunuliwa zaidi katika kupenda haki na kuchukia dhambi.Ebr.1:9.

          Kupenda kwake haki na kuchukia uwovu,ndiyo msingi wa Mungu kumpaka mafuta.Kwakufuata           msingi huu upako wa Mungu utafanya kazi juu ya maisha yetu.
          Kristo ni mfano wa kila mwamini hivyo ni lazima tuonyeshe sifa njema, na sio tofauti.Ebr.12:2.

4.UMEUMBWA ILI KUMTUMIKIA MUNGU.WARUMI 12:2.WAEFESO 2:10.

Pasipo nia zetu kufanywa upya,mwamini hawezi kujua wajibu wake katika Kristo.
ni kwa kutafakari neno na Roho mtakatifu.Mimi na wewe kama viungo katika mwili wa Kristo tunao wajibu wakufanya.I Kor.12:14-27.Unapokuwa huna chakufanya katka kanisa shetani atakupa kazi ya kufanya.Mfano tunaweza kuona kwa mfalme Daudi.II Sam.11:1-5.
Ukishindwa kumtumikia Mungu katika maisha yako lazima utamtumikia shetani..

5.UMEUMBWA KWA AJILI YA UTUME.MARKO 16:15-19.

Baada ya tu ya kuwa umeokoka,unalo jukumu la kuvuna roho za watu kwa kuwaleta kwa Kristo.Mith.11:30.

  • Yesu alituita sikumwendea tu bali pia na kwenda kwa wengine kwa ajili yake.Maneno ya Yesu ni maagizo kwa vizazi vyote kama ifuatavyo,

a.Kanisa linapaswa kuenenda ulimwenguni kote na kuhubiri injili kwa watu wote kwa msingi wa Neno    la Mungu.Efe.2:20.
b.Mahubiri yanapaswa kuelekezwa kwenye toba na msamaha.Lk.24:47.
c.Kusudi ni kuwa na wanafunzi wanaofuata maagizo ya Kristo.Yoh.8:31.Mk.1:17.


                     Kwa mafundisho zaidi karibu Beroya Christiani Centre.














Jumatatu, 11 Agosti 2014

KARIBU KATIKA SOMO LA KANUNI YA KUPANDA NA KUVUNA.WAGALATIA 6:7-9.MWANZO 8:22.

Dibaji:Maisha tunayoishi Yesu aliyafanananisha na ukulima.Mkulima anapolima na kupanda nia yake hasa ni kupata mavuno.Kama hunahaja ya kuvuna huna sababu ya kulima na kupata.
Tunahitaji kujua kwa kina namna gani maisha yetu ya wanaweza kuhusika katika kupanda na kuvuna itatusaidia kujihusisha katika kupanda mbegu njema ili kuvuna mavuno mema.
Aina za mbegu:
                      1.Sadaka maalum  2.Maneno 3.Mawazo 4.Matendo.
1.SADAKA MAALUM:2.Kor.9:6-11.Kuna aina tofauti tofauti ya upandaji, kadhalika katika kuvuna.
 a.Kupanda haba,kuvuna haba.Mungu atawabariki wa waamini sawa sawa na utoaji wao.Mith.11:24. Yeye azuiaye  anataka kumiliki kile alichonacho,hataki kuachilia au kutoa,ataelekea kwenye umasikini na ufukara.

 b.Kupanda kwa ukarimu: Nikupanda  mbegu nyingi na kuvuna kwa ukarimu. Kupanda ni kama kutawanya lakini kunakuongezewa. Mith.11:24. Wakati mwingine kupanda ni kama tendo la huzuni,lakini matekeo yake lakini matokeo ya kuvuna ni furaha kubwa.Zab.126:5-6.

 c.Kupanda kwa moyo mkunjufu: Haya huwa ni matokeo ya kujua nitavuna zaidi.Mungu humpenda mtu wa namna hii.2Kor.9:7.

 d.Kusudi la Mungu katika kutubariki: Mungu ndiye huwa anatoa mbegu za kupanda na mkate kwa mkulima.Moja ya sababu ya kukithili kwa uhitaji ni kwa sababu tunakula mbengu amabazo Mungu anataka tuzipande ili azizidishe. Ili tuzidi katika kala tendo njema na kufanyika baraka kwa wahitaji na wa kwaufalme wa Mungu. 2Kor.9:8-11.Mdo.9:36.
Matokeo ya utoaji huu.
-Wahitaji wanapata mahitaji yao
-Watoaji wanabarikiwa 
-Mungu anatukuzwa kwa shukrani.
Kuvuna ni hapa duniani.Mith.11:31.

2.MANENO YA KWINYWA CHAKO:
-Maneno ya kinywa chako huwa ni mbegu ambayo unaponena  ni kama unapanda kwa msingi wa kuvuna.
Mith.18:20-21.Kinywa kina uwezo wa kuzaa kile kisichokuwepo kikawepo.Maana ya mazao ya midomo ni kile kinachozaliwa na midomo.
-Vitu vyote tunavyoviona vimetoka na Neno la Mungu.Ebr.11:3.Ndani ya Uumbaji wote,kuna akili ,wazo,Neno,nguvu,na uhai wa Mungu.

 a.Utu wa ndani:Utu wako wa ndani ni kama Compyutar,chochote unachoingiza ndani ndicho kitakachotoka nje.Math.12:34-37.Kinywa chako kinatawala hatima ya maisha yako-
-Maneno ni kama chombo ya naweza kubeba upendo ,au chuki,mafanikio au umaskini,uzima au mauti.Yana weza kujenga au kubomoa,Hivyo tutavuna.

b.Jinsi ya kubadiri ukili Math.12:34.Nikujaza Neno la Mungu ndani ya moyo  wako.
-Kwa maana  kile unachojaza moyoni mwako ndicho kitakachotawala kinywa chako.Zab.119:11.Kol.3:16.
-Tunahitaji kumwomba Mungu aponye Vinywa vyetu.Zab.19:14.Isa.6:5.Yer.1:9.
-Jenga tabia ya kuisemea mema nafsi  yako siku zote.Zab.103:1-6.1Kor.14:28. Mifano ya watu waliopanda kwa vivywa vyao.-YAKOBO MWANZO 49. NUHU MWANZO 9:24-77.

3.MAWAZO YAKO NI MBEGU:ZAB. 19:14.
    1.Vipo vyanzo vikuu vitatu vya mawazo.
   a.Ulimwengu. Kutokana na unayoyaona na kuyasikia.Maneno huleta picha ya mambo katika akili zetu,na     zikatafakaliwa katika kuleta mawazo.
    b.Mwili.Kutoka na asili ya dhambi.Rum.8:5.
    c.Ibilisi.Kutokana na ulimwengu wa roho,mishale ya moto kwa leo ni mawazo mabaya kutoka kwa              shetani.Efeso.6:16
   2.Chanzo cha matatizo kwa  mtu huanzia ndani ya moyo.
   Math.4:23.Moyo usio safi ni chemchem ya uovu wa kila namna,na mtu hutiwa unajisi kwa hayo.Moyo        huwa kama kiwanda kinachozalisha uovu au wema. Math.15:18-19.Gal.5:19-23.Neno kumtia mtu      unajisi ,humaanisha,kutengwa na uzima,wokovu,na ushirika na Kristo.Zab.66:18.Mawazo ya sio                 matakatifu ya sipo pingwa,huweza kumwongoza mtu kwenye maneno na matendo yasiyo matakatifu.
   3.Jinsi ya kukabiliana na mawazo mabaya.BILLY GRAHAM. Mhubiri wa kimataifa      alisema,huwezi kuzuia ndege kuruka hewani ila unaweza kumzuia kujenga kioto  juu ya kichwa    chako.Akimaanisha huwezi kuzuia mawazo mabaya kuja kwenye ufahamu wako ila unaweza kuyapinga    kukaa kwenye ufahamu wako.
 Jenga tabia ya kupandikiza Neno la Mungu kwenye ufahamu wako,kwa kutafakari.Yosh.1:8.Zab.1:2-            4.Lifikie hatua ya kuwa sehemu ya utu wako wako ndani.
Kwa kutafakari Neno la Mungu,unajenga fikra zako na tabia pamoja na matendo yako katika msingi wa Neno la Mungu.
Kwakusoma Neno la Mungu na kufakari kuna maswali ya kujiuliza binafsi.Je,kuna ahadi hapa kwa ajiri yangu ili nidai? Je,kifungu hiki kinafunua dhambi nayopaswa kuiacha?Je,Mungu anatoa amri nayopaswa kuitii?Je,roho yangu inakubaliana na yale ambayo Roho anasema?Je,kifungu hiki kinaeleza ukweli juu ya Mungu,wokovu na dhambi duniani au utii wangu binafsi  na julishwa na Roho binafsi?

4.MATENDO YAKO NI MBEGU:MATH.7:12.
Kanuni ya kimsingi juu ya mafundisho ya kuhusu maadili.Inafundishwa kwa maneno  ya MATH.7:12.Maneno haya yanajumuisha mapenzi ya Mungu yaliyofunuliawa kupitia sheria na manabii yaani agano la kale lote.Math.22:37-40.Kauli hiyo inasisitiza umuhimu wa watu na mahusiano.
Hatupaswi kuepuka tu kuwadhulumu watu,lakini pia kuchukua hatua ya kuwasaidia wakati wa shida.Chochote unachopanda utakuwa wa kwanza kupata mavuno.2Tim.2:6.
a.Kipimo.Lk.6:37-38,Mith.22:8.Kipimo kiwe cha wema au uovu utakachompimia mtu mwingine ndicho na wewe utakachopimiwa.Kabla ya kufikiri kuwasaitia wengine kwanza tuchunguze maisha yetu kwanza.Wimbo.1:6,Lk.6:41-42.Usiwe mlinzi wa mashamba ya wengine lako ukasahau.
b.Mifano ya ki-Biblia.Kifo cha Naboth.1Fal.21:1-28.Kilikuwa cha hila baada ya kukataa kumuuzia shamba Mfalme Ahabu.Mkewe Ahabu akaanda mashitaka ya uongo dhidi yake akamuuwa yeye na watoto wake.mst.7-15.
Ujumbe wa Bwana kwa Ahabu mst.17-22.Matoke yake. 22:37-38.Kifo cha Yezeberli.11Falm.9:32-37.Vifo vya watoto wa Ahabu.IIFalm.10:6-10.
-Yonathani.
Wakati Mfalme Sauli alipotaka kumuuwa Daudi,Yonathani hakuwa tayari kwa hilo.Yeye alikuwa upande wa Daudi,mbegu aliyopanda kwa Daudi alikuja kuvuna mwanaye.IISam.9:1-8.
c.Ukumbusho mbele za Mungu.Matendo na maneno na sadaka huwa vinahifadhiwa katika kumbukumbu ya Mungu.
-Matendo.
Matendo mema au mabaya.Uf.14:13.20:11-15.
-Maneno.
Math.12:36-37.
-Sadaka na sala.Mdo.10:1-4.
Tusiache kutenda mema hayo ndiyo maisha ya Kikristo.Efe.2:10.Gal.6:9.

             KARIBU BEROYA CHRISTIAN CENTER KWA MAFUNDISHO ZAIDI.
                                                                                         

                              

Alhamisi, 7 Agosti 2014

KARIBU KATIKA KUYATAMBUA MAONO YA BEROYA CHRISTIAN CENTRE

MATHAYO 28:19-20. Basi,enendeni,mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi,mkiwabatiza kwa jina Baba, na Mwana,na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika  yote niliyowaamuru ninyi;na t
azama,mimi nipo pamoja nanyi siku zote,hata ukamilifu wa dahari.   

HILI NDILO AGIZO KUU, la  Bwana wetu Yesu Kristo ni agizo kuu kwa kanisa la  vizazi vyote. Kwatambu hili tunaweza kusema kuwa mafanikio ya Mchungaji yeyote hayapo kwakuwa na umati mkubwa wa watu anaoongoza.Bali kwa idadi ya watu aliowafanya kuwa wanafunzi Yesu kwakutii agizo hili.
LUKA 14:25-28.Tunamwona Yesu alipokuwa akifanya huduma yake chini ya jua,makutano mengi walimfuata lakini Yesu hakushawishika na hao makutano na kujivunia kuwa mimi nafuatwa na watu wengu nk.Kama ilivyo siku hizi wachungaji wengi wakijivunia makundi yao makubwa.
Katika AGANO JIPYA: Neno Mwanafunzi-kiyunani ni Mathetes-lipo mara 261.
Neno Mwamini-kiyunani ni Pistos-lipo mara 9.
Neno Mkristo-Kiyunani-christianos-lipo mara 3.
Wajibu wetu kama kanisa ni kuwafanya mataifa kuwa wanafunzi wa Yesu. Huundiyo wajibu tulionao hapa Beroya christian Centre:
1.Kuwafanya wasioamini kuwa waamini.

2.Waamini kuwa wanafunzi.

3.Wanafunzi kuwa viongozi.

4.Na viongozi kuwa viongozi wa viongozi.

5.Kuwafikia wasiofikiwa na Injili ya Kristo,ndani na nje ya nchi na kuanzisha makanisa katika maeneo hayo.

6.Kuandaa makongamano ya viongozi wa kiroho ndani na nje ya nchi ili kuwaimarisha na kuwajenga viongozi katika mwili wa Kristo juu ya msingi wa uanafunzi.

7.Kusaidia maskini,wajane,yatima,,wagonjwa kwa namna ambavyo Mungu atatuwezesha.

8.Kuanzisha vituo vya huduma za afya kama vile hosbital,dispensaries,nyumba kwa ajili ya watumishi na walemavu ambao watahudumiwa bule.

9.Kuanzisha miradi ya kimaendeleo na viwanda vidogovidogo vya kuwapa ujuzi waamini na wasio waamini ili waweze kujiajili wenyewe na kuendesha maisha yao.

10.Kuelimisha jamii kwa kutumia majarida,tracts,vitatabu,video,radio,television,semina,ushauri na maombezi.

HAPA BEROYA CHRISTIAN CENTRE TUNAMADARASA YA FUATAYO YA MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU:

Beroya under age 15.Darasa hili ni la watoto wa dogo,wanajengewa msingi wa kumpenda Mungu katika maisha yao na masomo mengine kwa mwaka mmoja.

Timothy class.Ni darasa la vijana wanaopevuka kuingia katika utu uzima.Mafudisho yake yanahusu kuwajengea msingi mzuri wa utumishi katika maisha yao.

Nazareth School of new believes.Darasa hili linahusika na mafundisho ya msingi baada ya mtu kumwamini Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake.Masomo yake ni ya mwaka mmoja.

Antiokia Class.Darasa hili ni la masomo ya msingi hatua ya pili baada ya wanafunzi kumaliza mwaka mmoja katika darasa la nazareth schhool of new believes,ndipo wanaingia katika darasa hili.

Tilano Class.Darasa hili ni la juu katika madarasa yetu,ni darasa la chuo cha Biblia linadumu kwa miaka miwili hadi mitatu.









Mch.Ezekiel & Anne joseph.
                                         KWA USHAURI NA MAOMBEZI:
                                         Ph.0755-305-794/0714-109-029,
                                         Email:mch.ezekiel@yahoo.com.

Jumanne, 5 Agosti 2014

KARIBU KATIKA KUUTAMBUA MSINGI WA IMANI WA BEROYA CHRISTIAN CENTRE

Biblia ndio mwongozo wetu wa imani na matendo katika maisha yetu ya Kikristo.Tamko hili ndilo msingi wa ushirika wetu .I.kor.1:10;Mdo2:42.Ukiri wa imani yetu ni kama ifuatavyo:

1.Maandiko Yaliyovuviwa:Maandiko ya Agano la kale na yale, ya Agano jipya, ya mevuviwa kihalisi na Mungu na ni ufunuo wa Mungu kwa mwanadamu, ni kiongozi cha imani kisicho shindwa wala kubadilika.2Tim. 3:15-17;1Thes 2:13;2Pet.1:2.

2.Mungu Mmoja aliye Hai na Kweli: Mungu mmoja tu aliye hai, aliye wa kweli na ambaye amekwisha jifunua  kama "MIMI NIKO"wa milele,muumbaji wa mbingu na nchi na Mkombozi wa Ulimwengu na Mwanadamu.Yeye kajifunua kama Baba ,Mwana na Roho Mtakatifu.Kumb.6:4; Isa.43:10,11:Mat.28:19;Lk.3:22.

3.Uungu wa Bwana Yesu:Bwana Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu na ana sifa zote za Uungu.Yoh.1:1;8:58;Isa.9:6;1Yoh.5:20
Maandiko yanatangaza:
   A.Kuzaliwa kwake na bikira Mat.1:23;Lk.1:31-35.
   B.Maisha yake yasiyo na dhambi Ebr.7:26;1Pet.2:22.
   C.Miujiza yake  Mdo.2:22,10:38.
   D.Kazi yake ya malipizi juu ya msalaba IKor,15:3,2Kor.5:21.
  E.Ufufuo wake kimwili kutoka katika wafu.Mat.28:6.Lk 24:39,Ikor.15:4.
  F.Kutukuzwa kwake kwenye mkono wa kiume wa Mungu.Mdo.1:9;11;2;33;Fil.2:9-11;Ebr.1;3.
4.Aguko la Mwanadamu : Mwanadamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu akiwa mzuri na mwema,
maana Mungu alisema "Natufanye Mtu kwa mfano wetu na sura yetu"Hata hivyo Mwanadanu kwa uasi wa hiyari yake mwenyewe alianguka  na kwa njia hiyo akajiletea sio mauti ya mwili tu,bali pia mauti ya kiroho ambayo ni kutengwa na Mungu.Mwa.1:26,27;2:17;3:6;Rum.5:12-19.

5.Wokovu wa Mwanadamu: Tumaini pekee la mwanadamu la Ukombozi ni kwa njia ya damu ya Yesu Kristo. Mwana wa Mungu iliyomwagika.

A.Masharti ya Wokovu: Wokovu hupatina kwa njia ya toba mbele za Mungu na imani kwa Bwana Yesu KristoKwa kuoshwa kwa kufanywa upya na kuzaliwa mara ya pili kwa njia ya Roho Mtakatifu,kuhesabiwa haki kwa neema kwa njia ya imani.Lk.24:47;Yoh.3:3;Rum.10:13-15;Tito.2:11;3:5-7;Efe.2:8.

B.Ushahidi wa Wokovu:Ushahidi wa Wokovu ulio wa ndani ni ushuhuda wa moja kwa moja wa Roho Mtakatifu.Rum.8:16.Ushahidi wa nje kwa  watu wote ni maisha ya haki na utakatifu wa kweli.Efe.4:24;Tito.2:12.

6.Maagizo ya kanisa:
A.Ubatizo katka Maji mengi: Agizo la ubatizo wa kuzamisha linatolewa  katika Maandiko. Wote wanaotubu na kumwamini Kristo kama Bwana na Mwokozi na Bwana wanaweza kubatizwa. Kwa njia  hiyo,wanautangazia ulimwengu kwamba wamekufa pamoja na kristo na pia kwamba wao wamefufuliwa pamoja naye ili kuenenda katika upya wa  uzima.Mat.28:19,Mk.16:6;Mdo.10:47,48;Rum.6:4.

B.Ushirika Mtakatifu: Meza ya Bwana ambayo ni mkate na matunda ya mzabibu ni mafano wa kuelezea ushirika wetu wa asili ya ki-Mungu na Bwana wetu Yesu Kristo.2Pet.1:4. Ni kumbukumbu ya mateso yake na kifo chake.1Kor.11:26. Na ni sharti wa waamini wote hata ajapo.

7.Ubatizo wa Roho Mtakatifu: Waamitini wote wanatakiwa na wanayo haki ya kutafuta ahadi ya Baba,yaani ubatizo wa Roho Mtakatifu na moto,kulingana na agizo la Bwana wetu Yesu Kristo.Huu ulikuwa ni ujuzi wa kawaida kwa wote waliokuwemo katika kanisa la mwanzo la Kikristo. Pamoja na huo ubatizo huja uwezo kutoka juu kwa ajili ya masha ya utumishi,na kutolewa kwa karama pamoja na matumizi yake katika huduma.Lk.24:24,49;Mdo.1:4;8; 1Kor.12:1-31. Ujuzi huu ni tofauti  kabisa ingawa unalingana na ujuzi wa kuzaliwa upya.Mdo.8:12-17,10:44-46;11:14-16;15:79.Pamoja na ujuzi huo wa ubatizo katika Roho Mtakatifu kunakuja ujuzi mwingine kama kujazwa mpaka kufurika kwa Roho Mtakatifu.Yoh.7:37-39,Mdo.4:8. Kumweshimu Mungu kwa undani zaidi.Mdo.2:43,Ebr.12:28,Kujitoa kwa hali ya juu kwa ajili ya Mungu na kujiweka wakfu kwa ajili ya kazi yake.Mdo.2:42,Pamoja na upendo  wenye vitendo zaidi kwa Kristo na kwa Neno lake na kwa waliopotea.Mk.16:20.


8.Ushahidi wa ubatizo katika Roho Mtakatifu:Ubatizo wa waamini katika Roho Mtakatifu unashuhudiwa kwa ishara ya nje iliyo ya kimwili ya kunena kwa lugha nyingine kama Roho wa Mungu anavyokujalia kutamka .Mdo. 2:4.Huku kusema kwa lugha ni sawa na ile karama ya aina za lugha .1Kor.12:4-10,28.Ingawa ni tofauti katika makusudi na matumizi.

9.Utakaso: Nitendo la kutengwa na kile kilicho kiovu na kujiweka wakfu kwa ajili ya Mungu.Rum.12:12;1Thes.5:23;Ebr.13:12.Maandiko yanatufundisha  juu ya maisha ya utakatifu ambayo pasipo huo hakuna atakaye mwona Mungu..Ebr.12:12-14.Kwa uwezo wa Roho Mtakatifu sisi tunao uwezo wa kutii amri ile."Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu" 1Pet.1:15,16. Utakaso huwa halisi katika mwamini kwa kugundua na kufahamu utambulisho wake na Kristo katika kifo chake na kufufuka kwake,na kwa imani akijihesabia kila mara kwamba yumo katika muungano huo,na kwa kutoa kila kiungo kwa utawala wa Roho Mtakatifu.Rum.6:1-11;13,8:12;13;Gal.2:20;Filp.2:12;13;1Pet.1:15.

10.Kanisa:Kanisa ni mwili wa Kristo, makao ya Mungu kwa njia ya Roho,lenye vyeo vya ki-Mungu  kwa ajili ya utimizo wa kazi yake kuu.Kila mwamini aliyezaliwa kwa Roho ni sehemu  muhimu ya kanisa ambalo ni kusanyiko la wazaliwa wa kwanza walioandikwa  Mbinguni.Efe.1:22;23;2:22;Ebr.12:23.

11.Huduma:Huduma ya ki-Mungu  pamoja na utumishi uliopangwa na Maandiko umetolewa na Bwana wetu kwa makusudi matano:
A.Kuushuhudia ulimwengu ulimwengu Mk.16:15-20.
B.Kujengwa kwa mwili wa kristo Efe.4:11-13.
C.Kuabudu Yoh.4:23-24.
D.Utumishi 1Kor.12;Rum.12;
E.Ushirika Mdo.2:42-46.

12.Uponyaji wa Mungu: Uponyaji wa Mungu nisehemu muhimu ya injili.Kufunguliwa kutoka magonjwa ni sehemu ni kitu kilichotoka katika malipizi na ni  haki ya kila anayeamini.Isa.53:4;5;Mat.8:16;17;Yak.5:14-16.

13.Tumaini lenye baraka: Ufufuo wa wale amabao wamelala katika Kristo na kunyakuliwa kwao pamoja nawale walio hai waliosalia mpaka wakati wakuja kwake Bwana ndilo tumaini lenye baraka na lililo kuu la kanisa. 1Thes.4:16,17; Rum.8:23;Tit.2:13;1Kor.15:51,52.

14.Utawala wa Kristo wa miaka Elfu:Kuja kwa mara ya pili kwa Kristo ni pamoja na kunyakuliwa  kwa Watakatifu ambalo ni tumainilenye baraka ,kukifuatiwa na kurudi kwa wazi kwa Kristo pamoja na Watakatifu wake kwa ajili ya utawala  hapa Ulimwenguni kwa muda wa miaka elfu moja.Zek.14:5;Mat.24:27;30;Ufu.1:7;19:11-14;20:1-6.Utawala huu wa miaka elfu moja utalewa wokovu kwa Israeli  kama taifa.Eze.37:21,22:8;Efe.3:19-20;Rum.11:26-27,na kuanzishwa kwa amani ya ulimwengu mzima.Isa.11:6-9,Zab.72:3-8,Mika.4:3-4.

15.Hukumu ya mwisho: Kutakuwepo na hukumu ya mwisho ambayo humo wafu waovu watafufuliwa na kuhukumiwa sawa sawa na matendo yao.Yeyote ambaye hatakuwa ameandikwa kaika kitabu cha uzima,pamoja na shetani na malaika zake,mnyama na nabii wa uongo,watatupwa katika adhabu ya milele katika ziwa liwakaalo moto na kibiriti,ambayo ni mauti ya pili.Mat.25:46;Mk.9:43-48;Ufu.19:20;20:11-15;21:8.

16.Mbingu Mpya na Nchi Mpya: Sisi,kulingana na ahadi yake tunatazamia mbingu mpya  na nchi  mpya ambamo haki ya kaa ndani yake.2Pet.3:13;Ufu.21:22.





Jumapili, 3 Agosti 2014

KARIBU KATIKA SOMO LA HATUA SABA KUELEKEA KWENYE USHINDI.II. MAMBO YA NYAKATI 20:1-38.WARUMI 8:37.


Dibaji:Hatuna haja ya kujifunza jinsi ya kubaki katika matatizo.Si siku zote utabaki katika hali ya matatizo.Dr.yongcho Alisema Wakristo sio wa kazi wa majangwani lakini wanaweza kupitia jangwani hatimaye wataingia kanani.Tunahitaji kujifunza jinsi ya kutoka katika hali ya kushinda na hatimaye kuingia katika ushindi.Kushindwa ni asili ya shetani na ushindi ni asili ya Mungu,asili hii ya Mungu huingia ndani ya watoto wa Mungu pale wanapomkubali na kumpokea Kristo kama Mwokozi.
HATUA YA KWANZA:Mtambue adui yako.II.Nyakati 20:1-2.
Huwezi kupambana na adui usiyemfahamu unahitaji kumtambua adui.Mfalme Yehoshati alitambua maadui waliokuja kupambana naye katika ufalme wake.
Wakristo tuna maadui watatu, yaani "Ulimwengu" "shetani"na "mwili wako".Hawa ni maadui wa kiroho.Mfumo wa Ulimwengu huu upo kinyume na kuamini kuokoka ndiyo maana unapotangaza kuwa umeoka baadhi yao wakuwa wanahisi umechanganyikiwa au umepoteza mwelekeo wa maisha.Ndiyo Biblia inasema tusiifuatishe dunia hii.Warumi 12:2.Shetani nia adui wa Mungu na adui wa kila mtu aliyemwamini Yesu,kazi zake zinaelezwa wazi katika Yohana 10:10.
Mwili ni adui ambaye unapomkemea yeye huwa yupo hakimbii yeye ndiye wewe.Mwili huwa hauna safari ya kwenda mbiguni bali nikaburini tu.Nia ya mwili ni mauti sawa na Warumi 8:5-8.
Ufahamu sahihi wa Neno la Mungu ni silaha kubwa ya kuweza kuwashinda hawa maadui.
HATUA YA PILI:Mtafute Bwana.II.Nyakati 20:3;II.Samweli 21:1.
Yehoshafati waliwaongoza Yuda katika maombi, kwa sababu alijua wazi kuwa Mungu ndiye mwenye majawabu yote tunayohitaji.Unawezaje kumtafuta Bwana? ni kwa kufunga na kuomba wakati mwingine unaweza kutafuta mahali pautulivu kama ni kwenye chumba  ukajifungia humo ili kupata muda na Bwana. kusoma Neno la Mu ngu kwenda katika ibada.Baadhi ya watu wanapokabiliwa na matatizo wana kwenda kwa waganga wa kienyeji au kutambikia mizimu kwa lengo la kupata uvumbuzi wa matatizo yao,mwisho wao umekuwa nikuishia katika huzuni na kuongeza matatizo badala ya majibu.Kuna nyakati tunapaswa kumtafuta Mungu ili kupata majibu ya shida zetu.mst 4-10.
HATUA YA TATU:Kubali kuwa wewe huna nguvu ya kutatua tatizo lako.II.Nyakati 20:1
2;Yohana 15:5.
Tatizo mengi tunayokabiliana nayo katika Umwengu huu hayana ufumbuzi katika nguvu za kimwili.Isipokuwa yanaufumbizi katika Mungu pekee.Mariko 4:35-41.Hapa tunaona Wanafunzi na Yesu wakivuka kwenda n'gambo kukatokea dhoruba kali,najaribu kuhisi inawezekana  wanafunzi kwa kutumia ujuzi wao wakivuvi walijaribu kukabiliana na dhoruba hii wa kashindwa.Ndipo wa kamwamsha Yesu.Yesu akakemea dhoruba ikakoma.Inawezekana kuna dhoruba katika masomo yako au familia huenda hata kazini kwako unachanganyikiwa bila kujua la kufanya.Kubali kuwa huna nguvu ya kutatua hilo tatizo lakini mwendee Mungu,mwenye nguvu zote za kutatua matatizo yote.Zekaria 4:6.
Unapoona unaweza kutatua matatizo yako Mungu huwa anakaa pembeni na kukuacha utatue kwa nguvu zako kama matoke utajikuta unashindwa.
HATUA YA NNE:Ondoa macho kwenye tatizo ya elekeze kwa Bwana.II.Nyakati 20:12.Zaburi 123:1-2.
Kwakadiri unavyokaza kaza macho kwenyetatizo,ndivyo adui anavyoendelea kulikuza kulikuza kwenye ufahamu wako.Nakamwe hutaona jibu la tatizo lako.
Mfano mzuri upo katika II.Wafalme 6:15-17.Kilichomfanya  mtumishi wa Elisha kuogopa na kupigayowe baada ya kuona kuona kuwa wamezungukwa na majeshi ya adui yaye alikaza macho kwenye tatizo badala ya kukaza macho kwenye jibu la tatizo.Kwanini tukaze macho kwa Bwana kwasababu ndiko kwenye ufumbuzi wa matatizo yetu.
Kilitokea nini wakati Stefano alipokaza macho kwa Mbiguni badala ya kukaza mamcho kwenye tatizo?Matendo 7:54-60.Aliona Utukufu wa Mungu na Mbingu zikiwa wazi.Wengi wameshindwa kuona Utukufu wa Mungu katika magumu wanayopitia kwa sababu tu wamekaza macho kwenye matatizo yao.
Mfano wa Petro katika Mathayo 14:22-33.Wakati Petro alipokuwa amekaza macho kwa Bwana alitembea bila kuzama juu ya maji,baada ya kuondoa macho kwa Bwana ndipo akanza kuzama.
Mara nyingi kuna kuzama kwingi katika maisha yetu ni kwa sababu ya kutoa macho kwa  Bwana.Kaza macho kwa BWANA.WAEBRANIA 12:2.
HATUA YA TANO:Starehe mbele za Bwana.II.Nyakati 14:15.
Baada ya kumwendea Mungu tuatatizoliache kwa Bwana usilibebe tena kwenye ufahamu kwako.I.Petro 5:6-7.Vita siyo yako ni ya Bwana.Wanadamu wanamiziko amabayo Yesu hataki waendelee kuibeba anataka kuwapa kupumnzika katika maisha yao.Mathayo 11:28-29.Sio mpango wa Mungu wewe siku zote uishi katika maisha ya shida ya matatizo ya siyoisha.II.Samweli 7:1.Tunaona Mfalme Daudi Bwana alistarehesha pande zote.Sasa ni wa kati wa Mungu kukustarehesha  kwa kujifunza hatua hizi saba na kuziweka katika matendo.
HATUA YA SITA:Msifu Bwana kabla ya vita unapokuwa vitani na baada ya vita.II.Nyakati 20:18
:19.
Sifa ni moja ya silaha kali dhidi ya shetani na majeshi yake.Ukisoma Zaburi 22:3-4.Sifa humtengenezea Mungu kiti cha Enzi katikati ya watu wake mahali pakuketi daima.
Maadu walishangaa kuona badala ya kukabiliana na wanajeshi walikabiliana na waimbaji!Bwana akainua waviziao hatimaye walipigana wao kwa wao na ushindi ukatokea.Mst.21-24.
HATUA YA SABA:Kushuhudia yale Bwana aliyotenda.II.Nyakati 20:26-30.
Kila mara Mungu anapotenda mambo makuu katika maisha yako usikae kimya shuhudia matendo makuu ya Bwana.Kunawengine huwa wanajengwa na shuhuda na mioyo yao kuinuliwa katika kumwamini Mungu kwa yale wanayotarajia kutoka kwa Bwana.Please!Hatukuitwa kutangaza kazi za shetani,shuhuda za kushidwa hatusitaki au za kuzimu nk.Zile zinazoelezea Ukuu wa Mungu.














Jumamosi, 2 Agosti 2014

kupitia uwanafunzi katika kristo tunamjua Mungu:

Mungu hujidhihirisha kupitia neno lake tu.Wala hatuna jinsi nyingine ya kumfahamu na kumjua Mungu nje ya neno lake hivyo inatupasa kujifunza sana neno lake.Wote waliofanikiwa kuishi na kutembea na Mungu katika maisha yao walikuwa na wanaendelea kuwa wanafunzi wazuri,uwanafunzi hauna kikomo kwani kamwe hatutafikia kikomo cha kumjua Mungu.Berea christian centre tunaamini juu ya uwanafunzi,tunauishi uwanafunzi kwa neno la Mungu na tumekuwa tukikutana na Mungu kwa jinsi ya kipekee sana.Blog hii itakusaidia kukusogeza karibu na Mungu kwa kukupatia mafundisho mbalimbali ya biblia katika nyanja tofautitofauti za maisha yako ya kiroho,kumbuka Mungu anakupenda sana na ana mpango na wewe,sasa ili kukamilisha kusudi la kimungu maishani mwako ni lazima ujifunze.

ZINGATIA:   kama huna mahusiano mazuri na yesu rudia maneno haya chini kwa kuyasoma ........

"Bwana yesu mimi ni mdhambi,ninakuja kwako kuanzia hivi sasa,unisamehe dhambi zangu zote,futa jina langu katika kitabu cha hukumu,andika jina
langu katika kitabu cha uzima wa milele,okoa roho yangu,nafsi na mwili wangu,nifanye kuwa mwanao kuanzia saa hii" 

Baada ya kuyasema maneno hayo kwa dhati na kumaanisha kuachana na maisha ya dhambi unakuwa umeingia katika ufalme wa bwana wetu yesu na umekuwa mtoto wa Mungu.
Beroya itakupatia mtiririko wa masomo ya siku,wiki,mwezi,mwaka.Mafundisho mbalimbali kama ya ndoa,vijana,uchumi na mengineyo mengi ya kiroho.Kwa muda mrefu kumekuwa na milipuko ya mafundisho yasiyo sahihi kiasi cha kuwapelekea watu kushindwa kujisimamia wanapokutana na matatizo maishani.Dawa ya matatizo yote inapatikana katika neno la Mungu lilobeba pumzi ya uhai wa kimungu.
www.facebook.com