Nivingumu kuthamini kitu usichojua uthamani wake.
Williamson alitemblea mwanduwi Shinyanga akawakuta wazee wa kisukuma wakicheza bao kwa kutumia vipande vya arimas,bila kujua wanachezea utajiri.Williamson akawazidi mahesabu hawa wazee ni kwasababu yeye alijua uthamani wa madini ya arimas.Alienda kuwanunulia groli za mvilingo zenye rangi ndani akawaomba,waupe hayo mawe ili awape groli mbazo ni nzuri zaidi kwa kuchezea bao.Wakampa bule akaenda kuuza uraya na kurudi na fedha nyingi na kununua eneo ambalo mpaka leo kuna machimbo ya madini.Huu ni mfano mzuri kwa wakristo wasiojua uthamani wa Neno hawana tofauti na wale wazee wa kisukuma.
Sasa twendwe kuchunguza kwa makini juu ya uthamani wa Neno la Mungu.
1.Neno la Mungu.Yoh.1:1.Maneno ya mtu hufunua moyo wake na mawazo yake.Kriso kama Neno alifunua,moyo na mawazo ya Mungu.Ebr.1:1-2.
Mungu leo anasema nasi kupitia Neno lake.
2.Neno linashikilia Uumbaji.Ebr.1:3;Mwa.1:1.Ebr.11:3.
3.Neno ni chakula cha mtu wa ndani.Yaani roho yako.roho yako inahitaji chakula cha Neno,kama mwili wako unavyohitaji chakula cha kawaida.Math.4:4;Ayu.23:12;Yer.15:16.
4.Kwa Neno tunazaliwa upya.Mwanadamu huwa anazaliwa mara mbili mara ya kwanza kupitia mahusiani ya wazazi wetu, mara ya pili ni kupitia Neno la Mungu.Efe.2:10,Ipet.1:23;Yak.1:18.IIKor.5:17.
5.Neno ni upanga wa Roho.Efe.6:17.Neno ni moja ya silaha yetu ya kushambulia adui.Kwa luhga nyingine ni silaha dhidi ya shetani.Uf.2:16;1:16;Math.4:4;7;10.
6.Neno linaponya.(nidawa)Tunaposimama katika Neno la Mungu tunapokea kile ambacho ni haki yetu.Mith.3:8;4:22,Zab.107:20,Math.8:8,13.Math.8:16.
7.Neno linatupa maisha malefu.Mith.3:2;4:10;22;9:11.Mungu alikusudia tuishi kulingana na Neno lake,nje ya Neno maisha yetu yanaweza kufupishwa na maisha ya dhambi.
8.Neno linatupa amani.Meth.3:2;Zab.120:165.
9.Neno linatupa hekima.Mtu aliyejaa Neno la Mungu ni mtu amabae hekima ya Mungu inaweza kuoneka kupitia yeye.Mith.2:1-6.
10.Neno litatupa ulinzi.Kupitia Neno tunakuwa salama.Zab.119:9.
11.Neno linatupa ushindi dhidi ya dhambi.Moyo usio na Neno ni kama nyumba isiyo na milango inakuwa haipo salama.Zab.119:9.
12.Neno linatupa mafanikio.Mungu anapo tubariki na kutuinua hayo yote huyafanya kwa msingi wa Neno lake,yeye hutenda kazi kwa msingi wa Neno.Yos.1:8;Zab.1:2-3.Math.7:24-27.
+Mambo ya kufanya katika kitabu cha torati.
-Kisiondoke vinywani mwetu
-Tutafakari maneno yake mchana na usiku.
-Tupate kutenda sawasawa na yaliyoandikwa humo.Math.25:31-46.
Matokeo yake ni kustawi kiroho na kimwili.
13.Neno linatufanya kuwa washirika wa tabia ya kiungu.IIPet.1:4.
14.Neno linatupa kila kinachotuongoza katika uzima na utauwa.IIPet.1:3.
15.Neno ni chanzo cha imani yetu.Imani yetu inachanzo katika Neno la Mungu,na inastawishwa na Neno la Mungu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni