Jumapili, 3 Agosti 2014
KARIBU KATIKA SOMO LA HATUA SABA KUELEKEA KWENYE USHINDI.II. MAMBO YA NYAKATI 20:1-38.WARUMI 8:37.
Dibaji:Hatuna haja ya kujifunza jinsi ya kubaki katika matatizo.Si siku zote utabaki katika hali ya matatizo.Dr.yongcho Alisema Wakristo sio wa kazi wa majangwani lakini wanaweza kupitia jangwani hatimaye wataingia kanani.Tunahitaji kujifunza jinsi ya kutoka katika hali ya kushinda na hatimaye kuingia katika ushindi.Kushindwa ni asili ya shetani na ushindi ni asili ya Mungu,asili hii ya Mungu huingia ndani ya watoto wa Mungu pale wanapomkubali na kumpokea Kristo kama Mwokozi.
HATUA YA KWANZA:Mtambue adui yako.II.Nyakati 20:1-2.
Huwezi kupambana na adui usiyemfahamu unahitaji kumtambua adui.Mfalme Yehoshati alitambua maadui waliokuja kupambana naye katika ufalme wake.
Wakristo tuna maadui watatu, yaani "Ulimwengu" "shetani"na "mwili wako".Hawa ni maadui wa kiroho.Mfumo wa Ulimwengu huu upo kinyume na kuamini kuokoka ndiyo maana unapotangaza kuwa umeoka baadhi yao wakuwa wanahisi umechanganyikiwa au umepoteza mwelekeo wa maisha.Ndiyo Biblia inasema tusiifuatishe dunia hii.Warumi 12:2.Shetani nia adui wa Mungu na adui wa kila mtu aliyemwamini Yesu,kazi zake zinaelezwa wazi katika Yohana 10:10.
Mwili ni adui ambaye unapomkemea yeye huwa yupo hakimbii yeye ndiye wewe.Mwili huwa hauna safari ya kwenda mbiguni bali nikaburini tu.Nia ya mwili ni mauti sawa na Warumi 8:5-8.
Ufahamu sahihi wa Neno la Mungu ni silaha kubwa ya kuweza kuwashinda hawa maadui.
HATUA YA PILI:Mtafute Bwana.II.Nyakati 20:3;II.Samweli 21:1.
Yehoshafati waliwaongoza Yuda katika maombi, kwa sababu alijua wazi kuwa Mungu ndiye mwenye majawabu yote tunayohitaji.Unawezaje kumtafuta Bwana? ni kwa kufunga na kuomba wakati mwingine unaweza kutafuta mahali pautulivu kama ni kwenye chumba ukajifungia humo ili kupata muda na Bwana. kusoma Neno la Mu ngu kwenda katika ibada.Baadhi ya watu wanapokabiliwa na matatizo wana kwenda kwa waganga wa kienyeji au kutambikia mizimu kwa lengo la kupata uvumbuzi wa matatizo yao,mwisho wao umekuwa nikuishia katika huzuni na kuongeza matatizo badala ya majibu.Kuna nyakati tunapaswa kumtafuta Mungu ili kupata majibu ya shida zetu.mst 4-10.
HATUA YA TATU:Kubali kuwa wewe huna nguvu ya kutatua tatizo lako.II.Nyakati 20:1
2;Yohana 15:5.
Tatizo mengi tunayokabiliana nayo katika Umwengu huu hayana ufumbuzi katika nguvu za kimwili.Isipokuwa yanaufumbizi katika Mungu pekee.Mariko 4:35-41.Hapa tunaona Wanafunzi na Yesu wakivuka kwenda n'gambo kukatokea dhoruba kali,najaribu kuhisi inawezekana wanafunzi kwa kutumia ujuzi wao wakivuvi walijaribu kukabiliana na dhoruba hii wa kashindwa.Ndipo wa kamwamsha Yesu.Yesu akakemea dhoruba ikakoma.Inawezekana kuna dhoruba katika masomo yako au familia huenda hata kazini kwako unachanganyikiwa bila kujua la kufanya.Kubali kuwa huna nguvu ya kutatua hilo tatizo lakini mwendee Mungu,mwenye nguvu zote za kutatua matatizo yote.Zekaria 4:6.
Unapoona unaweza kutatua matatizo yako Mungu huwa anakaa pembeni na kukuacha utatue kwa nguvu zako kama matoke utajikuta unashindwa.
HATUA YA NNE:Ondoa macho kwenye tatizo ya elekeze kwa Bwana.II.Nyakati 20:12.Zaburi 123:1-2.
Kwakadiri unavyokaza kaza macho kwenyetatizo,ndivyo adui anavyoendelea kulikuza kulikuza kwenye ufahamu wako.Nakamwe hutaona jibu la tatizo lako.
Mfano mzuri upo katika II.Wafalme 6:15-17.Kilichomfanya mtumishi wa Elisha kuogopa na kupigayowe baada ya kuona kuona kuwa wamezungukwa na majeshi ya adui yaye alikaza macho kwenye tatizo badala ya kukaza macho kwenye jibu la tatizo.Kwanini tukaze macho kwa Bwana kwasababu ndiko kwenye ufumbuzi wa matatizo yetu.
Kilitokea nini wakati Stefano alipokaza macho kwa Mbiguni badala ya kukaza mamcho kwenye tatizo?Matendo 7:54-60.Aliona Utukufu wa Mungu na Mbingu zikiwa wazi.Wengi wameshindwa kuona Utukufu wa Mungu katika magumu wanayopitia kwa sababu tu wamekaza macho kwenye matatizo yao.
Mfano wa Petro katika Mathayo 14:22-33.Wakati Petro alipokuwa amekaza macho kwa Bwana alitembea bila kuzama juu ya maji,baada ya kuondoa macho kwa Bwana ndipo akanza kuzama.
Mara nyingi kuna kuzama kwingi katika maisha yetu ni kwa sababu ya kutoa macho kwa Bwana.Kaza macho kwa BWANA.WAEBRANIA 12:2.
HATUA YA TANO:Starehe mbele za Bwana.II.Nyakati 14:15.
Baada ya kumwendea Mungu tuatatizoliache kwa Bwana usilibebe tena kwenye ufahamu kwako.I.Petro 5:6-7.Vita siyo yako ni ya Bwana.Wanadamu wanamiziko amabayo Yesu hataki waendelee kuibeba anataka kuwapa kupumnzika katika maisha yao.Mathayo 11:28-29.Sio mpango wa Mungu wewe siku zote uishi katika maisha ya shida ya matatizo ya siyoisha.II.Samweli 7:1.Tunaona Mfalme Daudi Bwana alistarehesha pande zote.Sasa ni wa kati wa Mungu kukustarehesha kwa kujifunza hatua hizi saba na kuziweka katika matendo.
HATUA YA SITA:Msifu Bwana kabla ya vita unapokuwa vitani na baada ya vita.II.Nyakati 20:18
:19.
Sifa ni moja ya silaha kali dhidi ya shetani na majeshi yake.Ukisoma Zaburi 22:3-4.Sifa humtengenezea Mungu kiti cha Enzi katikati ya watu wake mahali pakuketi daima.
Maadu walishangaa kuona badala ya kukabiliana na wanajeshi walikabiliana na waimbaji!Bwana akainua waviziao hatimaye walipigana wao kwa wao na ushindi ukatokea.Mst.21-24.
HATUA YA SABA:Kushuhudia yale Bwana aliyotenda.II.Nyakati 20:26-30.
Kila mara Mungu anapotenda mambo makuu katika maisha yako usikae kimya shuhudia matendo makuu ya Bwana.Kunawengine huwa wanajengwa na shuhuda na mioyo yao kuinuliwa katika kumwamini Mungu kwa yale wanayotarajia kutoka kwa Bwana.Please!Hatukuitwa kutangaza kazi za shetani,shuhuda za kushidwa hatusitaki au za kuzimu nk.Zile zinazoelezea Ukuu wa Mungu.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)