Ijumaa, 22 Agosti 2014

KARIBU KATIKA SOMO LA UANAFUNZI KAMA YESU ALIVYOFUNDISHA.MATHAYO 28:18-20.

Dibaji:Shauku ya Yesu nikuona kuwa wanapatikana wanafunzi katika mataifa yote.Katika lugha ya kiyunani Neno  enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi imeelezewa yaani ni kila kundi la kabila hapa duniani.Wajibu wetu ni kuwafanya watu kuwawanafunzi wanatii Neno la Mungu.
Mafanikio katika huduma hayapo katika wingi wa watu tulionao.Swali ni kwamba wangapi tumewaongoza kuwa wanafunzi wa Yesu?
Kinyume chake ni kushindwa,matokeo yake ni kuwa na mbuzi wengi kuliko kondoo.Mathayo 25:31-46.

YESU ANAFAFANUA UANAFUNZI: Yoh.8:31-32.
Uanafunzi ni hatua ya kwanza katika mahusiano na Mungu.Ina maana ni watu waliokubali kutubu dhambi zao na kumkubali Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao na kuwa tayari kutii Neno lake.
Wanafunzi wa kweli ni wale wanaokuwa tayari kudumu katika Neno lake.
Neno la kiyunani la mwanafunzi ni Mathetes-Linapatika mara 261 katika agano jipya.
Ambapo neno Mwamini  kiyunani Postos-Linapatika mara 9 katika agano jipya.Neno Mkristo kiyunani hupatika mara 3.
Kwa msingi huu sasa tunaweza kuhitimisha kuwa wale waliomwamini Bwana mwanzoni waliitwa wanafunzi.

VIGEZO VYA YESU JUU YA MWANAFUNZI.
1.Kuzaa matunda.Yoh.15:8-36.Tunapozaa matunda hilo huthibitisha kuwa sisi ni wanafunzi wa Yesu.Yapo matunda ya aina nyingi tunayopaswa kuzaa ila baadhi yake ni Tunda la Roho Mtakatifu tazama Gal.5:22-23.Tunda hili hufunua tabia ya Yesu katika maisha ya mwamini.Kwasababu hiyo ndilolinaleta tofauti kati yetu na wale ambao hawajaokoka.Mwamini anapozaa tunda la dhambi hiyo ni alama ya wazi kuwa hataokoka.Gal.5:19-21.Kuna matunda kama utumishi wetu kwa Bwana kuwaleta watu kwa Kristo na nk.Yoh.4:34-39.
2.Kuumpa Yesu nafasi ya kwanza katika ya mtu.Luka 14:25-26.Yoh.12:25.
Yesu hakulidhika na makutano mengi waliokuwa wakimfuata hakuwa kafikia lengo lake.Yesu anatafuta watu watakaompenda Mungu kwa mioyo yao yote akili,nafsi na nguvu zao,yaani wanafunzi.
Yesu hakuwa na maana ya kuwachukia wazazi wetu na ndugun zetu.Hii ni lugha ya kimfano,Yaani kama unataka kuwa mwanafunzi lazima tumpende yeye kuliko vyote.Mwanafunzi hutii na kushika amri zake yesu.Yoh.14:21.
3.Mtu yeyote asiyechukua msalaba wake.LukA 14:27.
Hapa pia anatumia lugha ya kimfano;kawaida ya warumi waliwasulubisha wahalifu kwenye kwenye njia kuu nje ya malango ya mji ili watu wengine waogope kufanya uhalifu."Beba msalaba wako"Msemo huu ulikuwa wakaida nyakati za Yesu.
Wahalifu waliogopa kusikia maneno  hayo,walijua ndiyo mwanzo wa saa ya mateso makali sana.
Msemo huu ulimaanisha =Kukabiliana na mateso magumu yanayokwijia ambayo hayaepukiki.
Mwanafunzi wa kweli yupo tayari kuteseka kwa ajili ya kumfuta Yesu.Flp.1:29.
Atakuwa tayari kuhesabu gharama.Luka 14:28,32.
Alichomaanisha Yesu ukitaka kuwa mwanafunzi wake,hesabu gharama mapema,ili usije ukakata tamaa mambao yatakapokuwa magumu.
4.Asiyeacha vyote alivyonavyo.Luka 14:33.Hii ni kauli ya kimfano;hakuwa na maana ya kuacha vyote tulivyonavyo tutaishije?Nilazima tuachilie kila kitu tulichonacho kwa maana ya kumkabidhi Mungu avimiliki na kufikia kiwango cha kutokutumikia mali,bali kumtumikia Mungu kwa mali zetu.
Kabla ya kufikiri kufanya wengine kuwa wanafunzi tunapaswa sisi wenyewe tuwe na hakika kuwa sisi ni wanafunzi.