Dibaji:Maisha tunayoishi Yesu aliyafanananisha na ukulima.Mkulima anapolima na kupanda nia yake hasa ni kupata mavuno.Kama hunahaja ya kuvuna huna sababu ya kulima na kupata.
Tunahitaji kujua kwa kina namna gani maisha yetu ya wanaweza kuhusika katika kupanda na kuvuna itatusaidia kujihusisha katika kupanda mbegu njema ili kuvuna mavuno mema.
Aina za mbegu:
1.Sadaka maalum 2.Maneno 3.Mawazo 4.Matendo.
1.SADAKA MAALUM:2.Kor.9:6-11.Kuna aina tofauti tofauti ya upandaji, kadhalika katika kuvuna.
a.Kupanda haba,kuvuna haba.Mungu atawabariki wa waamini sawa sawa na utoaji wao.Mith.11:24. Yeye azuiaye anataka kumiliki kile alichonacho,hataki kuachilia au kutoa,ataelekea kwenye umasikini na ufukara.
b.Kupanda kwa ukarimu: Nikupanda mbegu nyingi na kuvuna kwa ukarimu. Kupanda ni kama kutawanya lakini kunakuongezewa. Mith.11:24. Wakati mwingine kupanda ni kama tendo la huzuni,lakini matekeo yake lakini matokeo ya kuvuna ni furaha kubwa.Zab.126:5-6.
c.Kupanda kwa moyo mkunjufu: Haya huwa ni matokeo ya kujua nitavuna zaidi.Mungu humpenda mtu wa namna hii.2Kor.9:7.
d.Kusudi la Mungu katika kutubariki: Mungu ndiye huwa anatoa mbegu za kupanda na mkate kwa mkulima.Moja ya sababu ya kukithili kwa uhitaji ni kwa sababu tunakula mbengu amabazo Mungu anataka tuzipande ili azizidishe. Ili tuzidi katika kala tendo njema na kufanyika baraka kwa wahitaji na wa kwaufalme wa Mungu. 2Kor.9:8-11.Mdo.9:36.
Matokeo ya utoaji huu.
-Wahitaji wanapata mahitaji yao
-Watoaji wanabarikiwa
-Mungu anatukuzwa kwa shukrani.
Kuvuna ni hapa duniani.Mith.11:31.
2.MANENO YA KWINYWA CHAKO:
-Maneno ya kinywa chako huwa ni mbegu ambayo unaponena ni kama unapanda kwa msingi wa kuvuna.
Mith.18:20-21.Kinywa kina uwezo wa kuzaa kile kisichokuwepo kikawepo.Maana ya mazao ya midomo ni kile kinachozaliwa na midomo.
-Vitu vyote tunavyoviona vimetoka na Neno la Mungu.Ebr.11:3.Ndani ya Uumbaji wote,kuna akili ,wazo,Neno,nguvu,na uhai wa Mungu.
a.Utu wa ndani:Utu wako wa ndani ni kama Compyutar,chochote unachoingiza ndani ndicho kitakachotoka nje.Math.12:34-37.Kinywa chako kinatawala hatima ya maisha yako-
-Maneno ni kama chombo ya naweza kubeba upendo ,au chuki,mafanikio au umaskini,uzima au mauti.Yana weza kujenga au kubomoa,Hivyo tutavuna.
b.Jinsi ya kubadiri ukili Math.12:34.Nikujaza Neno la Mungu ndani ya moyo wako.
-Kwa maana kile unachojaza moyoni mwako ndicho kitakachotawala kinywa chako.Zab.119:11.Kol.3:16.
-Tunahitaji kumwomba Mungu aponye Vinywa vyetu.Zab.19:14.Isa.6:5.Yer.1:9.
-Jenga tabia ya kuisemea mema nafsi yako siku zote.Zab.103:1-6.1Kor.14:28. Mifano ya watu waliopanda kwa vivywa vyao.-YAKOBO MWANZO 49. NUHU MWANZO 9:24-77.
3.MAWAZO YAKO NI MBEGU:ZAB. 19:14.
1.Vipo vyanzo vikuu vitatu vya mawazo.
a.Ulimwengu. Kutokana na unayoyaona na kuyasikia.Maneno huleta picha ya mambo katika akili zetu,na zikatafakaliwa katika kuleta mawazo.
b.Mwili.Kutoka na asili ya dhambi.Rum.8:5.
c.Ibilisi.Kutokana na ulimwengu wa roho,mishale ya moto kwa leo ni mawazo mabaya kutoka kwa shetani.Efeso.6:16
2.Chanzo cha matatizo kwa mtu huanzia ndani ya moyo.
Math.4:23.Moyo usio safi ni chemchem ya uovu wa kila namna,na mtu hutiwa unajisi kwa hayo.Moyo huwa kama kiwanda kinachozalisha uovu au wema. Math.15:18-19.Gal.5:19-23.Neno kumtia mtu unajisi ,humaanisha,kutengwa na uzima,wokovu,na ushirika na Kristo.Zab.66:18.Mawazo ya sio matakatifu ya sipo pingwa,huweza kumwongoza mtu kwenye maneno na matendo yasiyo matakatifu.
3.Jinsi ya kukabiliana na mawazo mabaya.BILLY GRAHAM. Mhubiri wa kimataifa alisema,huwezi kuzuia ndege kuruka hewani ila unaweza kumzuia kujenga kioto juu ya kichwa chako.Akimaanisha huwezi kuzuia mawazo mabaya kuja kwenye ufahamu wako ila unaweza kuyapinga kukaa kwenye ufahamu wako.
Jenga tabia ya kupandikiza Neno la Mungu kwenye ufahamu wako,kwa kutafakari.Yosh.1:8.Zab.1:2- 4.Lifikie hatua ya kuwa sehemu ya utu wako wako ndani.
Kwa kutafakari Neno la Mungu,unajenga fikra zako na tabia pamoja na matendo yako katika msingi wa Neno la Mungu.
Kwakusoma Neno la Mungu na kufakari kuna maswali ya kujiuliza binafsi.Je,kuna ahadi hapa kwa ajiri yangu ili nidai? Je,kifungu hiki kinafunua dhambi nayopaswa kuiacha?Je,Mungu anatoa amri nayopaswa kuitii?Je,roho yangu inakubaliana na yale ambayo Roho anasema?Je,kifungu hiki kinaeleza ukweli juu ya Mungu,wokovu na dhambi duniani au utii wangu binafsi na julishwa na Roho binafsi?
4.MATENDO YAKO NI MBEGU:MATH.7:12.
Kanuni ya kimsingi juu ya mafundisho ya kuhusu maadili.Inafundishwa kwa maneno ya MATH.7:12.Maneno haya yanajumuisha mapenzi ya Mungu yaliyofunuliawa kupitia sheria na manabii yaani agano la kale lote.Math.22:37-40.Kauli hiyo inasisitiza umuhimu wa watu na mahusiano.
Hatupaswi kuepuka tu kuwadhulumu watu,lakini pia kuchukua hatua ya kuwasaidia wakati wa shida.Chochote unachopanda utakuwa wa kwanza kupata mavuno.2Tim.2:6.
a.Kipimo.Lk.6:37-38,Mith.22:8.Kipimo kiwe cha wema au uovu utakachompimia mtu mwingine ndicho na wewe utakachopimiwa.Kabla ya kufikiri kuwasaitia wengine kwanza tuchunguze maisha yetu kwanza.Wimbo.1:6,Lk.6:41-42.Usiwe mlinzi wa mashamba ya wengine lako ukasahau.
b.Mifano ya ki-Biblia.Kifo cha Naboth.1Fal.21:1-28.Kilikuwa cha hila baada ya kukataa kumuuzia shamba Mfalme Ahabu.Mkewe Ahabu akaanda mashitaka ya uongo dhidi yake akamuuwa yeye na watoto wake.mst.7-15.
Ujumbe wa Bwana kwa Ahabu mst.17-22.Matoke yake. 22:37-38.Kifo cha Yezeberli.11Falm.9:32-37.Vifo vya watoto wa Ahabu.IIFalm.10:6-10.
-Yonathani.
Wakati Mfalme Sauli alipotaka kumuuwa Daudi,Yonathani hakuwa tayari kwa hilo.Yeye alikuwa upande wa Daudi,mbegu aliyopanda kwa Daudi alikuja kuvuna mwanaye.IISam.9:1-8.
c.Ukumbusho mbele za Mungu.Matendo na maneno na sadaka huwa vinahifadhiwa katika kumbukumbu ya Mungu.
-Matendo.
Matendo mema au mabaya.Uf.14:13.20:11-15.
-Maneno.
Math.12:36-37.
-Sadaka na sala.Mdo.10:1-4.
Tusiache kutenda mema hayo ndiyo maisha ya Kikristo.Efe.2:10.Gal.6:9.
KARIBU BEROYA CHRISTIAN CENTER KWA MAFUNDISHO ZAIDI.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni