azama,mimi nipo pamoja nanyi siku zote,hata ukamilifu wa dahari.
HILI NDILO AGIZO KUU, la Bwana wetu Yesu Kristo ni agizo kuu kwa kanisa la vizazi vyote. Kwatambu hili tunaweza kusema kuwa mafanikio ya Mchungaji yeyote hayapo kwakuwa na umati mkubwa wa watu anaoongoza.Bali kwa idadi ya watu aliowafanya kuwa wanafunzi Yesu kwakutii agizo hili.
LUKA 14:25-28.Tunamwona Yesu alipokuwa akifanya huduma yake chini ya jua,makutano mengi walimfuata lakini Yesu hakushawishika na hao makutano na kujivunia kuwa mimi nafuatwa na watu wengu nk.Kama ilivyo siku hizi wachungaji wengi wakijivunia makundi yao makubwa.
Katika AGANO JIPYA: Neno Mwanafunzi-kiyunani ni Mathetes-lipo mara 261.
Neno Mwamini-kiyunani ni Pistos-lipo mara 9.
Neno Mkristo-Kiyunani-christianos-lipo mara 3.
Wajibu wetu kama kanisa ni kuwafanya mataifa kuwa wanafunzi wa Yesu. Huundiyo wajibu tulionao hapa Beroya christian Centre:
1.Kuwafanya wasioamini kuwa waamini.
2.Waamini kuwa wanafunzi.
3.Wanafunzi kuwa viongozi.
4.Na viongozi kuwa viongozi wa viongozi.
5.Kuwafikia wasiofikiwa na Injili ya Kristo,ndani na nje ya nchi na kuanzisha makanisa katika maeneo hayo.
6.Kuandaa makongamano ya viongozi wa kiroho ndani na nje ya nchi ili kuwaimarisha na kuwajenga viongozi katika mwili wa Kristo juu ya msingi wa uanafunzi.
7.Kusaidia maskini,wajane,yatima,,wagonjwa kwa namna ambavyo Mungu atatuwezesha.
8.Kuanzisha vituo vya huduma za afya kama vile hosbital,dispensaries,nyumba kwa ajili ya watumishi na walemavu ambao watahudumiwa bule.
9.Kuanzisha miradi ya kimaendeleo na viwanda vidogovidogo vya kuwapa ujuzi waamini na wasio waamini ili waweze kujiajili wenyewe na kuendesha maisha yao.
10.Kuelimisha jamii kwa kutumia majarida,tracts,vitatabu,video,radio,television,semina,ushauri na maombezi.
HAPA BEROYA CHRISTIAN CENTRE TUNAMADARASA YA FUATAYO YA MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU:
Beroya under age 15.Darasa hili ni la watoto wa dogo,wanajengewa msingi wa kumpenda Mungu katika maisha yao na masomo mengine kwa mwaka mmoja.
Timothy class.Ni darasa la vijana wanaopevuka kuingia katika utu uzima.Mafudisho yake yanahusu kuwajengea msingi mzuri wa utumishi katika maisha yao.
Nazareth School of new believes.Darasa hili linahusika na mafundisho ya msingi baada ya mtu kumwamini Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake.Masomo yake ni ya mwaka mmoja.
Antiokia Class.Darasa hili ni la masomo ya msingi hatua ya pili baada ya wanafunzi kumaliza mwaka mmoja katika darasa la nazareth schhool of new believes,ndipo wanaingia katika darasa hili.
Tilano Class.Darasa hili ni la juu katika madarasa yetu,ni darasa la chuo cha Biblia linadumu kwa miaka miwili hadi mitatu.
Mch.Ezekiel & Anne joseph. |
Ph.0755-305-794/0714-109-029,
Email:mch.ezekiel@yahoo.com.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni