Dibaji.Zaburi hii ni maelezo ya mtu ambaye moyo wake uimara katika Neno la Mungu.Hayumbishi na habari mbaya,moyo wake umethibitika ukimtumaini Bwana.Misingi huu unakupa ujasiri wa kukabiliana na yasiyotarajiwa katika maisha.Kukosa moyo thabiti katika Neno la Mungu ndipo unasikia leo watu wamekunywa sumu au kajinyonga ukichunguza chanzo cha matukio haya ni changamoto katika maisha.Kupitia somo hili tutakwenda kujifunza mambo ya msingi yanayoweza kuwa msaada mkubwa katika maisha yetu.
A.KUTAMBUA NYAKATI TUNAZOISHI LEO:
Nyaki hizi zinatoa mwangwa mkubwa kwa masumbufu,kuogopa,kutishwa kwa urahisi na habari mbaya.Mahali dhambi ilipo na neema inakuwepo kwa wingi.RUMI.5:20.
1.Mwamini anawezaje kuishi katika nyakati hizi?Anaweza kuishi moyo wake ukiwa imara ukimtumaini Bwana,pasipo kuogopa chochote kinachotokea duniani leo.Zab.112:8.
2.Kufikia kiwango cha mzaburi huyu.
Fika mahali pakutoenda kwa msukumo wowote,sikwa yale unayosikia au kuona.Moyo uliothabiti unajua kuwa Mungu anatosha na kuzidi naye atakutana na kila hitaji letu.Filp.4:19.
B.MOYO ULIOTHABITI UNAMTUMAINI BWANA.
Kama unatarajia kumtumaini Bwana lazima uamini Neno.Neno na Mungu ni kitu kimoja.RUMI.12:2;1Yoh.1:1.
1.Ishara za kurudi kwa Yesu na mwisho wa dunia.Math.24.Yesu alikuwa akifundisha kuhusu ishara za kurudi kwake hakusema siku au mwezi,mwaka nk.Yeye alitoa maelezo yanayohusu ishara zitakazo onyesha dalili za kurudi kwake na mwisho wa dunia.Yesu alifundisha katikati ya mashambulizi ya shetani hatupaswi kusumbuka,tunapaswa kuishi juu ya viwango vya dunia.
2.Mtu asiwadanganye.Math.24:4.
Yesu alitambua katikati ya hizo ishara za kurudi kwake,kutakuwa na mabomengi,yatakayo hubiriwa ambayo ambayo sio injili halisi.Mafundisho na mahubiri leo ni baraka yaani mafanikio ya kimwili tu.Yesu anakuwa kama mganga wa kienyeji anayefuatwa kwa lengo la kuwapa watu mafanikio kisha wafe waende motoni.Injili kuhusu toba,utakatifu ,wokovu imekuwa adimu kusikia.watu wanajua aina za baraka kuliko wanavyomjua mtoa baraka hizo.Kabla ya kuwahubiri watu baraka na mafanikio kwanza tuwahubiri mambo ya msingi kuhusu ufalme wa Mungu.
Niwajibu wa mwamini kutofautisha kati ya ukweli wa injili na mafundisho ya uongo.Mdo17:10-11.
3.Habari ya vita na matetesi ya vita{msitiswe}Math.42:6.
Lazima kutakuwa na njia ya kwetu ya kuishi katikati ya machafuko hayo.
4.Habari njema itahubiriwa.Math.24:14.Katikati ya habari mbaya na ngumu,kutakuwepo na mtu atakayesimama na kuhubiri habari njema.Ipo njia ya kuishi hapa duniani katika wakati huu pasipo kuogopa au kutupwa huko na huko na kila matatizo unayokutananayo.
Unaweza kujaa Neno la Mungu na kuwa imara.
C.MIFANO YA WATU WALIOKUWA NA MOYO THABITI.
1.Mtume Paulo.Rumi.8:31-39.Unaposoma mistari hii utaona ukiri wa mtu ambaye moyo wake ni thabiti katika Neno la Mungu.Wakati huu Paulo alikuwa anapitia kipindi kigumu cha vita bado alikuwa thabiti hakuona kitu cha kumtenga na upendo wa Mungu.Mapito ya Mtume Paulo.IIKor.11:22-32.
2.Mjenzi mwenye akili.Math.7:24-27.Anaelezea watu wa wili waliosikia Neno,mmoja alisikia na kutendea kazi Neno akawa imara katika Neno.Mwamba ni Neno.
Wapili alikia lakini hakutendea kazi Neno,akawa hana msingi,kwasabu hiyo hakuweza kuhimili dhoruba na mafuriko ya maisha.
Shetani atakuwa kwa urahisi ujenge msingi wa Neno la Mungu katika maisha yako.Ndiyo maana leo kunavita na ushindani mkubwa kwa waru kwenda kanisani na kujifun za Neno la Mungu,baadhi ya watu wanasoma Biblia jumapili kanisani,nyumbani akisoma anasinzia na kulala,watu wengi leo hawapendi kujifunza siri za mbinguni kupitia mafundisho ya Bilblia,wengi wanasinzia hadi katika ibada kanakwamba haikutosha walivyo lala vitandani mwao!kwenye biashara na maofini hawalali wala kusinzia hii ni ajabu.
Shetani atafanya kila awezalo kukuzuia kusonga mbele katika imani,ila kwa msaada wa Bwana tutashinda.Filp.4:13.
3.Yairo mkuu wa sinsgogi.Lk.8:40-42.Yairo aliamini moyoni mwake kwa Yesu kuweka mikono yake juu ya binti yake kuwa atapona na kuishi.Mk.5:12-35.Wakienda kwake mawanamke mwenyekutokwa na damu alikamatamwelekeo wa Yesu.Wakati Yesu akimuhudumia,wajumbe wakaja na kumweleza Yairo binti yako amakufa,kwa nini uendelee kumsumbua mwalimu?Hili lilikuwa kama shinikizo la shetani,Yairo akili kushindwa na kumlalamikia Yesu na yule mwanamke.
Katika mazingira kama haya wengi wamepoteza baraka za Mungu.Mk.11:24.Imani inasema ni vyangu sasa ,mazingira yanapinga kuwa huwezi kupokea.Kuna mazingira unaweza kusema Neno au kukaa kimya.Yesu hakusitushwa na habari ya wale wajumbe wa kushangaa.Jibu la Yesu usiogope amaini tu,mst.36.Mariko.Yesu anamtia moyo awe kama mzaburi wa Zabu.112.Asiyeogopa habari mbaya.Baada ya wajumbe kuja na habari mbaya kjwa kweli mazingira yalionekana kushindikana kabisa.Kutokushituliwa na habari mbaya huo ndiyo ulikuwa msingi na mwenendo wa maisha ya Yesu hapa duniani.
Matokeo yake binti alifufuka,moyo wake ulikuwa umethibitika kwa kile alichoamini.
4.Sababu ya wa kristo kunyan'ganywa baraka zao.
Nikwa sababu ya kushindwa kuliingiza Neno la Mungu katika mioyo yao na mioyo yao kuwa thabiti.
Mkristo mnyonge na dhaifu ni yule ambaye haelewi agano lake na Mungu.
Ikiwa utaripa Neno la Mnngu nafasi ya kwanza katika maisha yako na kuliweka juu ya vitu vyote,litaumba sura ya Yesu katika maisha yako au katika moyo wako.Utaona matokeo yale yale aliyoona Yesu akiwa hapa duniani.
Yesu hakuwahi kushindwa.Mwamini amevikwa vitu vile vile alivyokuwanavyo Yesu hapa duniani.Yaani Neno la Mungu lenye mamlaka yote.
M