Jumanne, 5 Agosti 2014

KARIBU KATIKA KUUTAMBUA MSINGI WA IMANI WA BEROYA CHRISTIAN CENTRE

Biblia ndio mwongozo wetu wa imani na matendo katika maisha yetu ya Kikristo.Tamko hili ndilo msingi wa ushirika wetu .I.kor.1:10;Mdo2:42.Ukiri wa imani yetu ni kama ifuatavyo:

1.Maandiko Yaliyovuviwa:Maandiko ya Agano la kale na yale, ya Agano jipya, ya mevuviwa kihalisi na Mungu na ni ufunuo wa Mungu kwa mwanadamu, ni kiongozi cha imani kisicho shindwa wala kubadilika.2Tim. 3:15-17;1Thes 2:13;2Pet.1:2.

2.Mungu Mmoja aliye Hai na Kweli: Mungu mmoja tu aliye hai, aliye wa kweli na ambaye amekwisha jifunua  kama "MIMI NIKO"wa milele,muumbaji wa mbingu na nchi na Mkombozi wa Ulimwengu na Mwanadamu.Yeye kajifunua kama Baba ,Mwana na Roho Mtakatifu.Kumb.6:4; Isa.43:10,11:Mat.28:19;Lk.3:22.

3.Uungu wa Bwana Yesu:Bwana Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu na ana sifa zote za Uungu.Yoh.1:1;8:58;Isa.9:6;1Yoh.5:20
Maandiko yanatangaza:
   A.Kuzaliwa kwake na bikira Mat.1:23;Lk.1:31-35.
   B.Maisha yake yasiyo na dhambi Ebr.7:26;1Pet.2:22.
   C.Miujiza yake  Mdo.2:22,10:38.
   D.Kazi yake ya malipizi juu ya msalaba IKor,15:3,2Kor.5:21.
  E.Ufufuo wake kimwili kutoka katika wafu.Mat.28:6.Lk 24:39,Ikor.15:4.
  F.Kutukuzwa kwake kwenye mkono wa kiume wa Mungu.Mdo.1:9;11;2;33;Fil.2:9-11;Ebr.1;3.
4.Aguko la Mwanadamu : Mwanadamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu akiwa mzuri na mwema,
maana Mungu alisema "Natufanye Mtu kwa mfano wetu na sura yetu"Hata hivyo Mwanadanu kwa uasi wa hiyari yake mwenyewe alianguka  na kwa njia hiyo akajiletea sio mauti ya mwili tu,bali pia mauti ya kiroho ambayo ni kutengwa na Mungu.Mwa.1:26,27;2:17;3:6;Rum.5:12-19.

5.Wokovu wa Mwanadamu: Tumaini pekee la mwanadamu la Ukombozi ni kwa njia ya damu ya Yesu Kristo. Mwana wa Mungu iliyomwagika.

A.Masharti ya Wokovu: Wokovu hupatina kwa njia ya toba mbele za Mungu na imani kwa Bwana Yesu KristoKwa kuoshwa kwa kufanywa upya na kuzaliwa mara ya pili kwa njia ya Roho Mtakatifu,kuhesabiwa haki kwa neema kwa njia ya imani.Lk.24:47;Yoh.3:3;Rum.10:13-15;Tito.2:11;3:5-7;Efe.2:8.

B.Ushahidi wa Wokovu:Ushahidi wa Wokovu ulio wa ndani ni ushuhuda wa moja kwa moja wa Roho Mtakatifu.Rum.8:16.Ushahidi wa nje kwa  watu wote ni maisha ya haki na utakatifu wa kweli.Efe.4:24;Tito.2:12.

6.Maagizo ya kanisa:
A.Ubatizo katka Maji mengi: Agizo la ubatizo wa kuzamisha linatolewa  katika Maandiko. Wote wanaotubu na kumwamini Kristo kama Bwana na Mwokozi na Bwana wanaweza kubatizwa. Kwa njia  hiyo,wanautangazia ulimwengu kwamba wamekufa pamoja na kristo na pia kwamba wao wamefufuliwa pamoja naye ili kuenenda katika upya wa  uzima.Mat.28:19,Mk.16:6;Mdo.10:47,48;Rum.6:4.

B.Ushirika Mtakatifu: Meza ya Bwana ambayo ni mkate na matunda ya mzabibu ni mafano wa kuelezea ushirika wetu wa asili ya ki-Mungu na Bwana wetu Yesu Kristo.2Pet.1:4. Ni kumbukumbu ya mateso yake na kifo chake.1Kor.11:26. Na ni sharti wa waamini wote hata ajapo.

7.Ubatizo wa Roho Mtakatifu: Waamitini wote wanatakiwa na wanayo haki ya kutafuta ahadi ya Baba,yaani ubatizo wa Roho Mtakatifu na moto,kulingana na agizo la Bwana wetu Yesu Kristo.Huu ulikuwa ni ujuzi wa kawaida kwa wote waliokuwemo katika kanisa la mwanzo la Kikristo. Pamoja na huo ubatizo huja uwezo kutoka juu kwa ajili ya masha ya utumishi,na kutolewa kwa karama pamoja na matumizi yake katika huduma.Lk.24:24,49;Mdo.1:4;8; 1Kor.12:1-31. Ujuzi huu ni tofauti  kabisa ingawa unalingana na ujuzi wa kuzaliwa upya.Mdo.8:12-17,10:44-46;11:14-16;15:79.Pamoja na ujuzi huo wa ubatizo katika Roho Mtakatifu kunakuja ujuzi mwingine kama kujazwa mpaka kufurika kwa Roho Mtakatifu.Yoh.7:37-39,Mdo.4:8. Kumweshimu Mungu kwa undani zaidi.Mdo.2:43,Ebr.12:28,Kujitoa kwa hali ya juu kwa ajili ya Mungu na kujiweka wakfu kwa ajili ya kazi yake.Mdo.2:42,Pamoja na upendo  wenye vitendo zaidi kwa Kristo na kwa Neno lake na kwa waliopotea.Mk.16:20.


8.Ushahidi wa ubatizo katika Roho Mtakatifu:Ubatizo wa waamini katika Roho Mtakatifu unashuhudiwa kwa ishara ya nje iliyo ya kimwili ya kunena kwa lugha nyingine kama Roho wa Mungu anavyokujalia kutamka .Mdo. 2:4.Huku kusema kwa lugha ni sawa na ile karama ya aina za lugha .1Kor.12:4-10,28.Ingawa ni tofauti katika makusudi na matumizi.

9.Utakaso: Nitendo la kutengwa na kile kilicho kiovu na kujiweka wakfu kwa ajili ya Mungu.Rum.12:12;1Thes.5:23;Ebr.13:12.Maandiko yanatufundisha  juu ya maisha ya utakatifu ambayo pasipo huo hakuna atakaye mwona Mungu..Ebr.12:12-14.Kwa uwezo wa Roho Mtakatifu sisi tunao uwezo wa kutii amri ile."Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu" 1Pet.1:15,16. Utakaso huwa halisi katika mwamini kwa kugundua na kufahamu utambulisho wake na Kristo katika kifo chake na kufufuka kwake,na kwa imani akijihesabia kila mara kwamba yumo katika muungano huo,na kwa kutoa kila kiungo kwa utawala wa Roho Mtakatifu.Rum.6:1-11;13,8:12;13;Gal.2:20;Filp.2:12;13;1Pet.1:15.

10.Kanisa:Kanisa ni mwili wa Kristo, makao ya Mungu kwa njia ya Roho,lenye vyeo vya ki-Mungu  kwa ajili ya utimizo wa kazi yake kuu.Kila mwamini aliyezaliwa kwa Roho ni sehemu  muhimu ya kanisa ambalo ni kusanyiko la wazaliwa wa kwanza walioandikwa  Mbinguni.Efe.1:22;23;2:22;Ebr.12:23.

11.Huduma:Huduma ya ki-Mungu  pamoja na utumishi uliopangwa na Maandiko umetolewa na Bwana wetu kwa makusudi matano:
A.Kuushuhudia ulimwengu ulimwengu Mk.16:15-20.
B.Kujengwa kwa mwili wa kristo Efe.4:11-13.
C.Kuabudu Yoh.4:23-24.
D.Utumishi 1Kor.12;Rum.12;
E.Ushirika Mdo.2:42-46.

12.Uponyaji wa Mungu: Uponyaji wa Mungu nisehemu muhimu ya injili.Kufunguliwa kutoka magonjwa ni sehemu ni kitu kilichotoka katika malipizi na ni  haki ya kila anayeamini.Isa.53:4;5;Mat.8:16;17;Yak.5:14-16.

13.Tumaini lenye baraka: Ufufuo wa wale amabao wamelala katika Kristo na kunyakuliwa kwao pamoja nawale walio hai waliosalia mpaka wakati wakuja kwake Bwana ndilo tumaini lenye baraka na lililo kuu la kanisa. 1Thes.4:16,17; Rum.8:23;Tit.2:13;1Kor.15:51,52.

14.Utawala wa Kristo wa miaka Elfu:Kuja kwa mara ya pili kwa Kristo ni pamoja na kunyakuliwa  kwa Watakatifu ambalo ni tumainilenye baraka ,kukifuatiwa na kurudi kwa wazi kwa Kristo pamoja na Watakatifu wake kwa ajili ya utawala  hapa Ulimwenguni kwa muda wa miaka elfu moja.Zek.14:5;Mat.24:27;30;Ufu.1:7;19:11-14;20:1-6.Utawala huu wa miaka elfu moja utalewa wokovu kwa Israeli  kama taifa.Eze.37:21,22:8;Efe.3:19-20;Rum.11:26-27,na kuanzishwa kwa amani ya ulimwengu mzima.Isa.11:6-9,Zab.72:3-8,Mika.4:3-4.

15.Hukumu ya mwisho: Kutakuwepo na hukumu ya mwisho ambayo humo wafu waovu watafufuliwa na kuhukumiwa sawa sawa na matendo yao.Yeyote ambaye hatakuwa ameandikwa kaika kitabu cha uzima,pamoja na shetani na malaika zake,mnyama na nabii wa uongo,watatupwa katika adhabu ya milele katika ziwa liwakaalo moto na kibiriti,ambayo ni mauti ya pili.Mat.25:46;Mk.9:43-48;Ufu.19:20;20:11-15;21:8.

16.Mbingu Mpya na Nchi Mpya: Sisi,kulingana na ahadi yake tunatazamia mbingu mpya  na nchi  mpya ambamo haki ya kaa ndani yake.2Pet.3:13;Ufu.21:22.