Jumanne, 12 Agosti 2014

KARIBU KATIKA SOMO LA KUGUNDUA KUSUDI LA MUNGU KWA KIJANA.KUTOKA 2:1-4.WAEBRANIA 11:24.

Dibaji.Upo umuhimu wa kugundua kusudi la Mungu katika maisha yako kama kijana,kwa sababu haupo duniani kwa bahati mbaya wewe sibahati mbaya hata kama wazazi wanaweza kusema walikuzaa kwa bahati mbaya,wao wanaweza kuona hivyo kwa sababu ya ufahamu wao wenye mipaka.Ila kwa Mungu sibahati mbaya.Mungu hanaga bahati mbaya wewe ni kusudi la Mungu wewe ni mpango wa Mungu,wewe ni ndoto ya Mungu.
Musa alizaliwa katika nchi ya Misri wakati wazazi wake wakiwa utumwani,kipindi alichozaliwa alikuta sheria imeshapitishwa kuuwawa kwa watoto wote wa kiume wanaozaliwa katika nchi ya Misri.Kwasababu yeye hakuzaliwa kwa bahati mbaya kama wewe msomaji wangu hakufa kwa sheria ya mfalme matokeo yake alikwenda kuishi katika nyumba ya mfalme yaliyetoa amri hiyo na kumlea kama mtoto wake.Akiandaliwa kuwa mfalme wa Misri,pamoja na yote aliyotendewa bado alijua kuwa yeye hakuwa mtoto wa Farao,kwa sababu alihitaji kusimama katika kusudi la Mungu.
Kutokugundua sababu ya kuwepo kwako duniani,utajikuta unaishi katika maisha ambayo ni kama mashua iliyo bahari isiyokuwa na mwelekeo.
Matokeo yake ni kutekwa na desturi mbaya za maisha ya dhambi.Kama vile ulevi,uzinzi,madawa ya kulevya,ujambazi nk.

  • Ni muhimu kujiuliza maswali haya:

         Je,wewe ni nani?
         Ndoto zako nini katika maisha?
         Una umuhimu gani kwa Baba yako na Mama yako,ndugu zako Taifa lako, kijiji chako?
         Wajibu wako katika jamii ni upi?
         Matarajio na malengo yako katika jamii ni yapi?
        Jamii yako inatarajia nini kutoka kwako?
        Je,mambo gani yanayodumisha ukamilifu wako,kimwili,kijamii,kisaikolojia,kiuchumi na kiroho?.

TUNAKWENDA KUJIFUNZA  SABABU TANO ZA KUWEPO KWAKO HAPA DUNIANI:
 Kila mwadamu mwenye akili timamu anahitaji kujitambua,kuna umuhimu mkubwa sana katika              kujitambu.Kama hujitambui huwezi kulinda uthamani wako.

1.UMEUMBWA ILI KUMPENDEZA MUNGU.KOLOSAI 1:16.

Lazima utambue kuwa umeubwa kwa ajili yake,Mungu.Wajibu wako ni  kumpenda Mungu.Kumpenda Mungu nikupenda anachopenda na kuchukia anachochukia.Mwaanzo 39:9.
Kwasabubu hiyo kila kitu kinachokuhusu kinapaswa kuanza na Mungu na kuishia na Mungu.
Hili hudhihilishwa na kumwabudu Mungu na kuwa na ushirikiano naye.Huu ndiyo wito wetu  mkuu.KUTOKA 3:12.Kama huwezi kumwabudu Mungu pia huwezi kumpendeza na hata kumtumikia.Yoh.4:23-24.Math.4:8-10.
Kuabudu ni zaidi ya kwenda jumapili kanisani,kunahusu mfumo mzima wa maisha yetu kaika kuishi kama atakavyo yeye.

2.UMEUMBWA ILI UWESEHEMU YA FAMILIA YA MUNGU.YOHANA 1:12.

Naweza kusema kuwa hapa duniani kuna makundi mawili ya watu,watoto wa Mungu na watu wa Mungu.Ebr.2:10,Yoh.1:12.Ili kuwa mtoto wa Mungu ni pale unapo mkubali Kristo kuwa Bwana na Mwokozi katika maisha.Kinyume chake utabaki kuwa mtu wa Mungu.Mpango wa Mungu wa kuwa na familia ulikuwepo kabla ujazaliwa.
Huwezi kuwa nje ya Yesu na bado ukawa sehemu ya familia ya Mungu.Kanisa hatujiungi kama klabu bali kwa kuzaliwa upya.Yoh.3:3.
Biblia inafunua wazi kuwa kunafamilia mbili ya shetani na ya Mungu.Yoh.8:44.Umepewa uamuzi wa kuchugua kuwa familia ya Mungu au ya shetani.

3.UMEUBWA ILI UFANANE NA KRISTO.WARUMI 8:29.

   Kusudi kuu la wokovu ni kutuleta katika  kufanana Kristo.Kwa maana ya Kristo kuonekana katika        maisha yetu.IKor.11:1.
                         
          Ni nini maana ya kufanana na Kristo? I Yoh.2:6. 

  • Kufanana na Kristo ni kumpenda Mungu na kuwapenda watu wengine.Math.22:37;IYoh.4:20-21.Upendo wa Mungu kwa waamini hutuchochea kuwapenda watu wengine.
  • Pendo hudai uaminifu wetu kwa Mungu.Ebr.3:2.

           Tunamwona Yesu akiwa tayari kuyatimiza mapenzi ya Mungu kwa kutoa maisha yake kwa                    ukombozi wetu.Math.26:42.Tunapaswa kuwa waaminifu kutimiza mapenzi yake bila kujari                  ghalama.

  • Pendo la Kristo lilifunuliwa zaidi katika kupenda haki na kuchukia dhambi.Ebr.1:9.

          Kupenda kwake haki na kuchukia uwovu,ndiyo msingi wa Mungu kumpaka mafuta.Kwakufuata           msingi huu upako wa Mungu utafanya kazi juu ya maisha yetu.
          Kristo ni mfano wa kila mwamini hivyo ni lazima tuonyeshe sifa njema, na sio tofauti.Ebr.12:2.

4.UMEUMBWA ILI KUMTUMIKIA MUNGU.WARUMI 12:2.WAEFESO 2:10.

Pasipo nia zetu kufanywa upya,mwamini hawezi kujua wajibu wake katika Kristo.
ni kwa kutafakari neno na Roho mtakatifu.Mimi na wewe kama viungo katika mwili wa Kristo tunao wajibu wakufanya.I Kor.12:14-27.Unapokuwa huna chakufanya katka kanisa shetani atakupa kazi ya kufanya.Mfano tunaweza kuona kwa mfalme Daudi.II Sam.11:1-5.
Ukishindwa kumtumikia Mungu katika maisha yako lazima utamtumikia shetani..

5.UMEUMBWA KWA AJILI YA UTUME.MARKO 16:15-19.

Baada ya tu ya kuwa umeokoka,unalo jukumu la kuvuna roho za watu kwa kuwaleta kwa Kristo.Mith.11:30.

  • Yesu alituita sikumwendea tu bali pia na kwenda kwa wengine kwa ajili yake.Maneno ya Yesu ni maagizo kwa vizazi vyote kama ifuatavyo,

a.Kanisa linapaswa kuenenda ulimwenguni kote na kuhubiri injili kwa watu wote kwa msingi wa Neno    la Mungu.Efe.2:20.
b.Mahubiri yanapaswa kuelekezwa kwenye toba na msamaha.Lk.24:47.
c.Kusudi ni kuwa na wanafunzi wanaofuata maagizo ya Kristo.Yoh.8:31.Mk.1:17.


                     Kwa mafundisho zaidi karibu Beroya Christiani Centre.