Jumatatu, 25 Agosti 2014

KARIBU KATIKA SOMO LA VITA VYA KIROHO.2KORINTHO 10:3-5.EFESO 6:12.

Dibaji:Kama waamini tunaitaji kujua kuwa tunavita, katika ulimwengu huu tunaoishi kuna aina mbili ya falme kuna ufalme wa giza na ufalme wa nuru.Ufalme wa giza unatawaliwa na shetani na mapepo yake na ufalme wa nuru unatawaliwa na Yesu Kristo.Kwahiyo vita hii inahusisha watu waliyoko chini ya ufalme wa Mungu dhidi ya ufalme wa giza.Unapomkubali Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wako moja kwa moja unakuwa adui wa ufalme wa shetani.Sasa kama waamini tunahitaji kujifunza namna gani tunaweza kukabiliana na vita hivi!Lazima tujue tunayomamlaka  juu ya shetani na majeshi yake.Vita hivi ni vya kiroho sio vya kimwili.Uwanja  mkubwa wa mapambano ni kwenye  mawazo au akili zetu.Shetani hupandikiza mawazo mabaya  ndani yetu,yanayopingana na Neno la Mungu na mapenzi ya Mungu.

A.MUUNDO WA UTAWALA SHETANI  WA SHETANI:WAEFESO 6:10-13.
1.Shetani.
Shetani ni mkuu wa utawala wa giza Biblia ina mwita mfalme wa uwezo waanga.Efeso 2:2.
2.Falme.
Falme ni mashetani wa wakilishi wa utawala wa shteni wanaotawala falme kubwa,kimfano mabara kama vile africa,africa mashariki, ulaya ,asia na nk.
3.Wenyemamlaka.
Wenyemamlaka ni mashetani yanayotawala nchi,kupitia tawala za wanadamu.
4.Wakuu wa giza.
Nimashetani yanayotawala manbo ya giza ya kishetani kimfano,uendelezwaji wa dhambi,umaskini,ujinga na magonjwa.
5.Majeshi ya pepo wabaya.
Yanaitwa majeshi kwasababu yapo mengi na yote hayana kazi moja yanafanya kazi kama vikosi vikosi.Kama vile katika mataifa yetu tunamajeshi yaliyogawanyika katika utendaji tofauti tofauti.
6.Binadamu wanaomtumikia  shetani walioingia mkataba au agano na shetani ili kumtumikia.Kama vile wachawi,maajenti nk.

B.SILAHA ZETU ZA KUJIHAMI{KUJILINDA}EFESO 6:10-18.
1.Chepeo ya wokovu{kofia}kolosai 1:13.
Chepeo ilikuwa silaha yaani kofia ya chuma iliyovaliwa na askari wa kirumi kuhifadhi kichwa na mashambulizi ya adui.Kiroho chepeo ya wokovu,hulinda akili zetu kutokana na mashambulizi ya shetani.{Kujua ukombozi wako katika Kristo ni ulinzi}
2.Dirii ya haki kifuani.
Dirii ya haki ili kuwani ni fulana ambazo risasi haiwezi kupenya.{bullet proof vest}
Waamini ambao hawajapata ufahamu wa haki ya Kristo wameacha roho zao wazi kwa ajili ya kushindwa.
Tumepewa haki ya Yesu kama zawadi sio kwa kustahili kwetu bali kwa neema yake tu.
Sasa tunao wajibu wa kuishi katika haki kwa kutii neno la Mungu.2Kor.5:21.Nikama mfano raia wa nchi 
asiyejua haki zake kama raia nilahisi kupoteza hazako za msingi.Mafundisho mengi leo kuhusu kuvunjiwa laana na kufanyiwa maombi ya ukombozi,mengi ya hayo yamejengwa katika msingi wakutokujua haki zetu ndani ya Kristo kupitia msalaba wake.
3.Kweli viunoni.
Huu ulikuwa ni aina ya mkanda ulifungwa kiunoni,kumsaidia askari mavazi yake kushikamanishwa vizuri na mwili wake na kutokupata shida awapo vitani.Kiroho kweli hii ni tabia  ya Mungu ambayo kwa mwamini hufanyika silaha ya kujilinda.Kwasababu adui hana hiyo kweli.Tabia hii inampa mwamini ujasiri wa kukabiliana na kila changamoto katika maisha yake ya imani.
4.Utayari wa injili ya amani.
Utayari wa kutumika  hiyo ni silaha kali dhidi ya adui.2Tim 4:2.Unapokuwa unasukumwa sukumwa ili kumtumikia Mungu ujue unapoteza silaha yako dhidi ya adui.Kumbuka shetani na majeshi yake wanafanya kazi kwa bidii usiku na mchana,hapotesi kila fursa inayotokea mbele yake.
5.Ngao ya imani.
Askari wa wakati ule alitumia ngao iliyokuwa ngozi ya mnyama ilitengenezwa kwa mfano wa kama vile ungo ili kuzuia mishale yenye moto isimdhuru mpiganaji.
Imani hufanyika kama uzio wetu wa ulinzi ili kuzima mishale yenye moto.
C.SILAHA ZETU ZA KUSHAMBULIA.
1.Upanga wa Roho{Neno la Mungu}
Tunaweza kufanya kufanya mashambulizi kwa kutumia Neno la Mungu.Ufu.1:16;2:16.Ebr.4:12.Kwa maana hii sasa tunahitaji kulihamisha Neno la Mungu katika kurasa za Biblia na kuliweka ndani ya mioyo yetu,linapotoka ndani ya mioyo yetu kupitia vinywa vyetu huitwa upanga wa Roho.Hii ndiyo silaha ambayo Yesu alitumia ili kumshambulia shetani na hatimaye kumshinda.Math.4:4-11.
2.Jina la Yesu.
Unapompokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wako unapewa haki ya uwakili wa kutumia Jina la Yesu.Yoh.16:23-24,Uf.19:13.Kwa kutamka Jina la Yesu unaweza kuharibu kazi zote za shetani.
3.Imani ni silaha ya kujilinda na kushambulia.1Yoh.5:4.Imani ni njia Yetu ya ushindi dhidi ya ya ulimwengu.
4.Kuomba katika roho yaani kunena kwa lugha ni silaha yenye nguvu.
 -Ina mjenga mwamini na kumwimalisha
 -Maana ya kujenga ni kuinua,kufanya jasiri,kutia nguvu mpya.1Kor.14:4.
5.Sifa.
Sifa ni silaha yenye nguvu dhidi ya adui.
 -Sifa humtukuza Mungu
 -Sifa humsimamisha na kumzima shetani.Zab.8 na 9.
D.MADHAIFU YA SHETANI.
 Ufunguo kwa ushindi katika.
Kujua udhaifu wa adui yako,unakuwa na asilimia kubwa ya kushinda.Shetani huwa anatusoma maeneo yetu ya udhaifu na kushambulia hayo maeneo.
1.Hawezi kutenda kazi katikati ya sifa.Zab.22:3.
Sifa humsimamisha na kumnyamazisha adui.Huteka na kuzishinda ngazi zote za majeshi ya adui.
2.Hawezi kutenda kazi wakati Neno la Mungu limenenwa.Uf.1:16.
3.Hawezi kufanya kazi katika Jina la Yesu kwa sababu limeinuliwa juu ya majina yote.Flp.2:8-11.
4.Hawezi kufanya kazi katika upendo kwa sababu yeye asili yake ni chuki.1Kor.13:13.
5.Hawezikunya kazi katika nuru.Kwasababu yeye ni giza.Zab.119:105.
 -Neno liingiapo,huleta nuru au mwangaza.Zab.119:130.
 -Unaposimamia  Neno la Mungu ni sawa na kama umewasha mwangwa wa taa makali.
6.Hawezi kufanya kazi mahali penye kweli.Neno ndiyo kweli.Yoh.17:17,8:44.
7.Hawezi kufanya kazi wakati Neno la Mungu limepewa mamlaka ya kwanza na ya mwisho katika maisha yako.Yoh.6:68.



















Ijumaa, 22 Agosti 2014

KARIBU KATIKA SOMO LA UANAFUNZI KAMA YESU ALIVYOFUNDISHA.MATHAYO 28:18-20.

Dibaji:Shauku ya Yesu nikuona kuwa wanapatikana wanafunzi katika mataifa yote.Katika lugha ya kiyunani Neno  enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi imeelezewa yaani ni kila kundi la kabila hapa duniani.Wajibu wetu ni kuwafanya watu kuwawanafunzi wanatii Neno la Mungu.
Mafanikio katika huduma hayapo katika wingi wa watu tulionao.Swali ni kwamba wangapi tumewaongoza kuwa wanafunzi wa Yesu?
Kinyume chake ni kushindwa,matokeo yake ni kuwa na mbuzi wengi kuliko kondoo.Mathayo 25:31-46.

YESU ANAFAFANUA UANAFUNZI: Yoh.8:31-32.
Uanafunzi ni hatua ya kwanza katika mahusiano na Mungu.Ina maana ni watu waliokubali kutubu dhambi zao na kumkubali Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao na kuwa tayari kutii Neno lake.
Wanafunzi wa kweli ni wale wanaokuwa tayari kudumu katika Neno lake.
Neno la kiyunani la mwanafunzi ni Mathetes-Linapatika mara 261 katika agano jipya.
Ambapo neno Mwamini  kiyunani Postos-Linapatika mara 9 katika agano jipya.Neno Mkristo kiyunani hupatika mara 3.
Kwa msingi huu sasa tunaweza kuhitimisha kuwa wale waliomwamini Bwana mwanzoni waliitwa wanafunzi.

VIGEZO VYA YESU JUU YA MWANAFUNZI.
1.Kuzaa matunda.Yoh.15:8-36.Tunapozaa matunda hilo huthibitisha kuwa sisi ni wanafunzi wa Yesu.Yapo matunda ya aina nyingi tunayopaswa kuzaa ila baadhi yake ni Tunda la Roho Mtakatifu tazama Gal.5:22-23.Tunda hili hufunua tabia ya Yesu katika maisha ya mwamini.Kwasababu hiyo ndilolinaleta tofauti kati yetu na wale ambao hawajaokoka.Mwamini anapozaa tunda la dhambi hiyo ni alama ya wazi kuwa hataokoka.Gal.5:19-21.Kuna matunda kama utumishi wetu kwa Bwana kuwaleta watu kwa Kristo na nk.Yoh.4:34-39.
2.Kuumpa Yesu nafasi ya kwanza katika ya mtu.Luka 14:25-26.Yoh.12:25.
Yesu hakulidhika na makutano mengi waliokuwa wakimfuata hakuwa kafikia lengo lake.Yesu anatafuta watu watakaompenda Mungu kwa mioyo yao yote akili,nafsi na nguvu zao,yaani wanafunzi.
Yesu hakuwa na maana ya kuwachukia wazazi wetu na ndugun zetu.Hii ni lugha ya kimfano,Yaani kama unataka kuwa mwanafunzi lazima tumpende yeye kuliko vyote.Mwanafunzi hutii na kushika amri zake yesu.Yoh.14:21.
3.Mtu yeyote asiyechukua msalaba wake.LukA 14:27.
Hapa pia anatumia lugha ya kimfano;kawaida ya warumi waliwasulubisha wahalifu kwenye kwenye njia kuu nje ya malango ya mji ili watu wengine waogope kufanya uhalifu."Beba msalaba wako"Msemo huu ulikuwa wakaida nyakati za Yesu.
Wahalifu waliogopa kusikia maneno  hayo,walijua ndiyo mwanzo wa saa ya mateso makali sana.
Msemo huu ulimaanisha =Kukabiliana na mateso magumu yanayokwijia ambayo hayaepukiki.
Mwanafunzi wa kweli yupo tayari kuteseka kwa ajili ya kumfuta Yesu.Flp.1:29.
Atakuwa tayari kuhesabu gharama.Luka 14:28,32.
Alichomaanisha Yesu ukitaka kuwa mwanafunzi wake,hesabu gharama mapema,ili usije ukakata tamaa mambao yatakapokuwa magumu.
4.Asiyeacha vyote alivyonavyo.Luka 14:33.Hii ni kauli ya kimfano;hakuwa na maana ya kuacha vyote tulivyonavyo tutaishije?Nilazima tuachilie kila kitu tulichonacho kwa maana ya kumkabidhi Mungu avimiliki na kufikia kiwango cha kutokutumikia mali,bali kumtumikia Mungu kwa mali zetu.
Kabla ya kufikiri kufanya wengine kuwa wanafunzi tunapaswa sisi wenyewe tuwe na hakika kuwa sisi ni wanafunzi.
















Jumanne, 19 Agosti 2014

KARIBU KATIKA SOMO LA KANUNI ZA IMANI ZILETAZO MATOKEO.ZABURI 89:34;MALAKI 3:6.

Dibaji:Mungu aliwambia Israeli MIMI NI MUNGU NISIYEBADIRIKA.Neno la Mungu huwa halibadiriki ili kuendandana na mazingira.Inamaana mazingira yeyote hatakama nimagumu yakiwa nje ya uwezo wetu kama wanadamu bado hayawezi kulibadiri Neno la Mungu.
Mungu huwa habadiriki ila yeye huwa ana sifa ya kubadilisha.Mungu hadhuriki na chochote kinachoendelea Ulimwenguni huu.
Unaweza kumtegemea Mungu ambaye akisema amesema yeye huwabadilishi kauli yake.Nitofauti na wanadamu ambao leo wanaweza kusema bila kutekeleza walichosema.
Kwakutambua kanuni hizi humfanya mwamini awe na imani isiyoyumba katika Mungu wake.Kwasababu hiyo hupokea mahitaji yake.
A.TAFUTA AHADI KATIKA NENO LA MUNGU KWA KILE UNACHOHITAJI.
Mungu wetu anaishi ndani ya Neno lake na anatenda kazi kwa msingi wa Neno,hakuna njia ya kukutana na Mungu ila ni kwa msingi wa Neno lake.
Kunambo mawili amambayo kamwe hayawezi kubadilishwa au kubadirika.WABRANIA 6:13-18.ZABURI 138:2.
 1.Ahadi za Mungu
 2.Kiapo cha Mungu
-SHIDA YA WAKRISTO WENGI NI KWAMBA:
 1.Hawazijui hizo ahadi
 2.Hawaamini hata wanapozijua
 3.Wanakaza macho sana  kwa shetani na yale anayosema

B.LIAMINI NENO LA MUNGU.
TITO 1:2;HESABU 23:19.Kwasababu Mungu hawezi kusema uongo,anachosema kwako atafanya.
Nilini na kwa namna gani hilo huwajibikinalo.Wewe unawajibika na kumwamini,kuwa hawezi kusema uongo.
1.Wewe unawajibika alichosema nini kisha..
2.Uwe na uhakika wa ndani  kabisa kuwa hawezi kudanganya.Mashaka ni kikwazo kikubwa cha kupokea kutoka kwa Mungu.Mk.9:23.

C.USIFIKIRI HALI ZINAZOONEKANA KUPINGANA.IIKor.4:18.
Yakitambo=ya muda tu yaani siyoyakudumu.Kwa lugha nyingine mambo yenyeuwezekano wa kubadirika.Chochote unachokiona kwa macho yako hicho si chakudumu,kipo katika hali ya kubadirika.
Badilisha mtazamo wako juu ya matatizo,majaribu ya napokuja Mungu pia huja kwa msaada wake.
Mf.Lk.8:41-50.Ukisoma Maandiko haya utaona hapa kuwa mazingira yaliyopingana kabisa, lakini bado Mungu alifanya muujiza.
Angalia jawabu la tatizo badala ya kutafakari tatizo lenyewe.IIFalm 6:8-16.
Lione Neno kama linakidhi kikamilifu kukuvusha kwenye tatizo hilo.
1.Ulitambue tatizo
2.Usitafakari wala usiendelee kuliangalia
3.Usiendelee kulizungumuzia.Kuna baadhi ya watu hata wakisha mwomba Mungu bado wanakuwa wakizungumuzia tatizo hilo kila wanapokwenda.
4.Nenda kwenye Neno la Mungu ambalo imani yako hutokea.
5.Jibu hilotatizo ukisimama katika Neno la Mungu.Mk.11:23.Mlima utaondoka kwa kuumbia sio kwa kuutazama tu na kusikitika.
6.Ona yasiyoonekana kwa jicho la IMANI.Imani ni jicho la imani kuona yale yasiyoonekena kwa macho ya kimwili.
D.MSIFU MUNGU KWA AJILI YA JIBU.ZAB.119:89.ZAB.150:1.
Imba kwa imani msifu Mungu kwa jibu hata kama hujaliona kwa macho ya kimwili.
























Jumamosi, 16 Agosti 2014

KARIBU KATIKA SOMO LA MOYO ULIOTHABITI.ZABURI 112:7-8;125:1.

Dibaji.Zaburi  hii ni maelezo ya mtu ambaye moyo wake uimara katika Neno la Mungu.Hayumbishi na habari mbaya,moyo wake umethibitika ukimtumaini Bwana.Misingi huu unakupa ujasiri wa kukabiliana na yasiyotarajiwa katika maisha.Kukosa moyo thabiti katika Neno la Mungu ndipo unasikia leo watu wamekunywa sumu au kajinyonga ukichunguza chanzo cha matukio haya ni changamoto katika maisha.Kupitia somo hili tutakwenda kujifunza mambo ya msingi yanayoweza kuwa msaada mkubwa katika maisha yetu.
A.KUTAMBUA NYAKATI TUNAZOISHI LEO:
Nyaki hizi zinatoa mwangwa mkubwa kwa masumbufu,kuogopa,kutishwa kwa urahisi na habari mbaya.Mahali dhambi ilipo na neema inakuwepo kwa wingi.RUMI.5:20.
1.Mwamini anawezaje kuishi katika nyakati hizi?Anaweza kuishi moyo wake ukiwa imara ukimtumaini Bwana,pasipo kuogopa chochote kinachotokea duniani leo.Zab.112:8.
2.Kufikia kiwango cha mzaburi huyu.
Fika mahali pakutoenda kwa msukumo wowote,sikwa yale unayosikia au kuona.Moyo uliothabiti unajua kuwa Mungu anatosha na kuzidi naye atakutana na kila hitaji letu.Filp.4:19.

B.MOYO ULIOTHABITI UNAMTUMAINI BWANA.
Kama unatarajia kumtumaini Bwana lazima uamini Neno.Neno na Mungu ni kitu kimoja.RUMI.12:2;1Yoh.1:1.
1.Ishara za kurudi kwa Yesu na mwisho wa dunia.Math.24.Yesu alikuwa akifundisha kuhusu ishara za kurudi kwake hakusema siku au mwezi,mwaka nk.Yeye alitoa maelezo yanayohusu ishara zitakazo onyesha dalili za kurudi kwake na mwisho wa dunia.Yesu alifundisha  katikati ya mashambulizi ya shetani hatupaswi kusumbuka,tunapaswa kuishi juu ya viwango vya dunia.
2.Mtu asiwadanganye.Math.24:4.
Yesu alitambua  katikati ya hizo ishara za kurudi kwake,kutakuwa na mabomengi,yatakayo hubiriwa ambayo ambayo sio injili halisi.Mafundisho na mahubiri leo ni baraka yaani mafanikio ya kimwili tu.Yesu anakuwa kama mganga wa kienyeji anayefuatwa kwa lengo la kuwapa watu mafanikio kisha wafe waende motoni.Injili kuhusu toba,utakatifu ,wokovu imekuwa adimu kusikia.watu wanajua aina za baraka kuliko wanavyomjua mtoa baraka hizo.Kabla ya kuwahubiri watu baraka na mafanikio kwanza tuwahubiri mambo ya msingi kuhusu ufalme wa Mungu.
Niwajibu wa mwamini kutofautisha kati ya ukweli wa injili na mafundisho ya uongo.Mdo17:10-11.
3.Habari ya vita na matetesi ya vita{msitiswe}Math.42:6.
Lazima kutakuwa na njia ya kwetu ya kuishi katikati ya machafuko hayo.
4.Habari njema itahubiriwa.Math.24:14.Katikati ya habari mbaya na ngumu,kutakuwepo na mtu atakayesimama na kuhubiri habari njema.Ipo njia ya kuishi hapa duniani katika wakati huu pasipo kuogopa au kutupwa huko na huko na kila matatizo unayokutananayo.
Unaweza kujaa Neno la Mungu na kuwa imara.
C.MIFANO YA WATU WALIOKUWA NA MOYO THABITI.
1.Mtume Paulo.Rumi.8:31-39.Unaposoma mistari hii utaona ukiri wa mtu ambaye moyo wake ni thabiti katika Neno la Mungu.Wakati huu Paulo alikuwa anapitia kipindi kigumu cha vita bado alikuwa thabiti hakuona kitu cha kumtenga na upendo wa Mungu.Mapito ya Mtume Paulo.IIKor.11:22-32.
2.Mjenzi mwenye akili.Math.7:24-27.Anaelezea watu wa wili waliosikia Neno,mmoja alisikia na kutendea kazi Neno akawa imara katika Neno.Mwamba ni Neno.
Wapili alikia lakini hakutendea kazi Neno,akawa hana msingi,kwasabu hiyo hakuweza kuhimili dhoruba na mafuriko ya maisha.
Shetani atakuwa kwa urahisi ujenge msingi wa Neno la Mungu katika maisha yako.Ndiyo maana leo kunavita na ushindani mkubwa kwa waru kwenda kanisani na kujifun za Neno la Mungu,baadhi ya watu wanasoma Biblia jumapili kanisani,nyumbani akisoma anasinzia na kulala,watu wengi leo hawapendi kujifunza siri za mbinguni kupitia mafundisho ya Bilblia,wengi wanasinzia hadi katika ibada kanakwamba haikutosha walivyo lala vitandani mwao!kwenye biashara na maofini hawalali wala kusinzia hii ni ajabu.
Shetani atafanya kila awezalo kukuzuia kusonga mbele katika imani,ila kwa msaada wa Bwana tutashinda.Filp.4:13.
3.Yairo mkuu wa sinsgogi.Lk.8:40-42.Yairo aliamini moyoni mwake kwa Yesu kuweka mikono yake juu ya binti yake kuwa atapona na kuishi.Mk.5:12-35.Wakienda kwake mawanamke mwenyekutokwa na damu alikamatamwelekeo wa Yesu.Wakati Yesu akimuhudumia,wajumbe wakaja na kumweleza Yairo binti yako amakufa,kwa nini uendelee kumsumbua mwalimu?Hili lilikuwa kama shinikizo la shetani,Yairo akili kushindwa na kumlalamikia Yesu na yule mwanamke.
Katika mazingira kama haya wengi wamepoteza baraka za Mungu.Mk.11:24.Imani inasema ni vyangu sasa ,mazingira yanapinga kuwa huwezi kupokea.Kuna mazingira unaweza kusema Neno au kukaa kimya.Yesu hakusitushwa na habari ya wale wajumbe wa kushangaa.Jibu la Yesu usiogope amaini tu,mst.36.Mariko.Yesu anamtia moyo awe kama mzaburi wa Zabu.112.Asiyeogopa habari mbaya.Baada ya wajumbe kuja na habari  mbaya kjwa kweli mazingira yalionekana kushindikana kabisa.Kutokushituliwa na habari mbaya  huo ndiyo ulikuwa msingi na mwenendo wa maisha ya Yesu hapa duniani.
Matokeo yake binti alifufuka,moyo wake ulikuwa umethibitika kwa kile alichoamini.
4.Sababu ya wa kristo kunyan'ganywa baraka zao.
Nikwa sababu ya kushindwa kuliingiza Neno la Mungu katika mioyo yao na mioyo yao kuwa thabiti.
Mkristo mnyonge na dhaifu ni yule ambaye haelewi agano lake na Mungu.
Ikiwa utaripa Neno la Mnngu nafasi ya kwanza katika maisha yako na kuliweka juu ya vitu vyote,litaumba sura ya Yesu  katika maisha yako au katika moyo wako.Utaona matokeo yale yale aliyoona Yesu akiwa hapa duniani.
Yesu hakuwahi kushindwa.Mwamini amevikwa vitu vile vile alivyokuwanavyo Yesu hapa duniani.Yaani Neno la Mungu lenye mamlaka yote.

















M



Alhamisi, 14 Agosti 2014

KARIBU KATIKA KATIKA SOMO LA UTHAMANI WA NENO LA MUNGU.IITIMOTHEO 3:16-17.YOHANA 6:63.

Dibaji:Mafundisho ya msingi lazima ya jengwe katika maisha ya mwamini hili litampa mwamini nguvu ya ushindi.Kutoelewa uthamani wa Neno la Mungu,hatimaye nikuwa na maisha duni ya kiroho.
Nivingumu kuthamini kitu usichojua uthamani wake.
Williamson alitemblea mwanduwi Shinyanga akawakuta wazee wa kisukuma wakicheza bao kwa kutumia vipande vya arimas,bila kujua wanachezea utajiri.Williamson akawazidi mahesabu hawa wazee ni kwasababu yeye alijua uthamani wa madini ya arimas.Alienda kuwanunulia groli za mvilingo zenye rangi ndani akawaomba,waupe hayo mawe ili awape groli mbazo ni nzuri zaidi kwa kuchezea bao.Wakampa bule akaenda kuuza uraya na kurudi na fedha nyingi na kununua eneo ambalo mpaka leo kuna  machimbo ya madini.Huu ni mfano  mzuri kwa wakristo wasiojua uthamani wa Neno hawana tofauti na wale wazee wa kisukuma.
 Sasa twendwe kuchunguza kwa makini juu ya uthamani wa Neno la Mungu.
1.Neno la Mungu.Yoh.1:1.Maneno ya mtu hufunua moyo wake na mawazo yake.Kriso kama Neno alifunua,moyo na mawazo ya Mungu.Ebr.1:1-2.
Mungu leo anasema nasi kupitia Neno lake.
2.Neno linashikilia Uumbaji.Ebr.1:3;Mwa.1:1.Ebr.11:3.
3.Neno ni chakula cha mtu wa ndani.Yaani roho yako.roho yako inahitaji chakula cha Neno,kama mwili wako unavyohitaji chakula cha kawaida.Math.4:4;Ayu.23:12;Yer.15:16.
4.Kwa Neno tunazaliwa upya.Mwanadamu huwa anazaliwa mara mbili mara ya kwanza kupitia mahusiani ya wazazi wetu, mara ya pili ni kupitia Neno la Mungu.Efe.2:10,Ipet.1:23;Yak.1:18.IIKor.5:17.
5.Neno ni upanga wa Roho.Efe.6:17.Neno ni moja ya silaha yetu ya kushambulia adui.Kwa luhga nyingine ni silaha dhidi ya shetani.Uf.2:16;1:16;Math.4:4;7;10.
6.Neno linaponya.(nidawa)Tunaposimama katika Neno la Mungu tunapokea kile ambacho ni haki yetu.Mith.3:8;4:22,Zab.107:20,Math.8:8,13.Math.8:16.
7.Neno linatupa maisha malefu.Mith.3:2;4:10;22;9:11.Mungu alikusudia tuishi kulingana na Neno lake,nje ya Neno maisha yetu yanaweza kufupishwa na maisha ya dhambi.
8.Neno linatupa amani.Meth.3:2;Zab.120:165.
9.Neno linatupa hekima.Mtu aliyejaa Neno la Mungu  ni mtu amabae hekima ya Mungu inaweza kuoneka kupitia yeye.Mith.2:1-6.
10.Neno litatupa ulinzi.Kupitia Neno tunakuwa salama.Zab.119:9.
11.Neno linatupa ushindi dhidi ya dhambi.Moyo usio na Neno ni kama nyumba isiyo na milango inakuwa haipo salama.Zab.119:9.
12.Neno linatupa mafanikio.Mungu anapo tubariki na kutuinua hayo yote huyafanya kwa msingi wa Neno lake,yeye hutenda kazi kwa msingi wa Neno.Yos.1:8;Zab.1:2-3.Math.7:24-27.
+Mambo ya kufanya katika kitabu cha torati.
   -Kisiondoke vinywani mwetu
   -Tutafakari maneno yake mchana na usiku.
   -Tupate kutenda sawasawa na yaliyoandikwa humo.Math.25:31-46.
Matokeo yake ni kustawi kiroho na kimwili.
13.Neno linatufanya kuwa washirika wa tabia ya kiungu.IIPet.1:4.
14.Neno linatupa kila kinachotuongoza katika uzima na utauwa.IIPet.1:3.
15.Neno ni chanzo cha imani yetu.Imani yetu inachanzo katika Neno la Mungu,na inastawishwa na Neno la Mungu.

















Jumanne, 12 Agosti 2014

KARIBU KATIKA SOMO LA KUGUNDUA KUSUDI LA MUNGU KWA KIJANA.KUTOKA 2:1-4.WAEBRANIA 11:24.

Dibaji.Upo umuhimu wa kugundua kusudi la Mungu katika maisha yako kama kijana,kwa sababu haupo duniani kwa bahati mbaya wewe sibahati mbaya hata kama wazazi wanaweza kusema walikuzaa kwa bahati mbaya,wao wanaweza kuona hivyo kwa sababu ya ufahamu wao wenye mipaka.Ila kwa Mungu sibahati mbaya.Mungu hanaga bahati mbaya wewe ni kusudi la Mungu wewe ni mpango wa Mungu,wewe ni ndoto ya Mungu.
Musa alizaliwa katika nchi ya Misri wakati wazazi wake wakiwa utumwani,kipindi alichozaliwa alikuta sheria imeshapitishwa kuuwawa kwa watoto wote wa kiume wanaozaliwa katika nchi ya Misri.Kwasababu yeye hakuzaliwa kwa bahati mbaya kama wewe msomaji wangu hakufa kwa sheria ya mfalme matokeo yake alikwenda kuishi katika nyumba ya mfalme yaliyetoa amri hiyo na kumlea kama mtoto wake.Akiandaliwa kuwa mfalme wa Misri,pamoja na yote aliyotendewa bado alijua kuwa yeye hakuwa mtoto wa Farao,kwa sababu alihitaji kusimama katika kusudi la Mungu.
Kutokugundua sababu ya kuwepo kwako duniani,utajikuta unaishi katika maisha ambayo ni kama mashua iliyo bahari isiyokuwa na mwelekeo.
Matokeo yake ni kutekwa na desturi mbaya za maisha ya dhambi.Kama vile ulevi,uzinzi,madawa ya kulevya,ujambazi nk.

  • Ni muhimu kujiuliza maswali haya:

         Je,wewe ni nani?
         Ndoto zako nini katika maisha?
         Una umuhimu gani kwa Baba yako na Mama yako,ndugu zako Taifa lako, kijiji chako?
         Wajibu wako katika jamii ni upi?
         Matarajio na malengo yako katika jamii ni yapi?
        Jamii yako inatarajia nini kutoka kwako?
        Je,mambo gani yanayodumisha ukamilifu wako,kimwili,kijamii,kisaikolojia,kiuchumi na kiroho?.

TUNAKWENDA KUJIFUNZA  SABABU TANO ZA KUWEPO KWAKO HAPA DUNIANI:
 Kila mwadamu mwenye akili timamu anahitaji kujitambua,kuna umuhimu mkubwa sana katika              kujitambu.Kama hujitambui huwezi kulinda uthamani wako.

1.UMEUMBWA ILI KUMPENDEZA MUNGU.KOLOSAI 1:16.

Lazima utambue kuwa umeubwa kwa ajili yake,Mungu.Wajibu wako ni  kumpenda Mungu.Kumpenda Mungu nikupenda anachopenda na kuchukia anachochukia.Mwaanzo 39:9.
Kwasabubu hiyo kila kitu kinachokuhusu kinapaswa kuanza na Mungu na kuishia na Mungu.
Hili hudhihilishwa na kumwabudu Mungu na kuwa na ushirikiano naye.Huu ndiyo wito wetu  mkuu.KUTOKA 3:12.Kama huwezi kumwabudu Mungu pia huwezi kumpendeza na hata kumtumikia.Yoh.4:23-24.Math.4:8-10.
Kuabudu ni zaidi ya kwenda jumapili kanisani,kunahusu mfumo mzima wa maisha yetu kaika kuishi kama atakavyo yeye.

2.UMEUMBWA ILI UWESEHEMU YA FAMILIA YA MUNGU.YOHANA 1:12.

Naweza kusema kuwa hapa duniani kuna makundi mawili ya watu,watoto wa Mungu na watu wa Mungu.Ebr.2:10,Yoh.1:12.Ili kuwa mtoto wa Mungu ni pale unapo mkubali Kristo kuwa Bwana na Mwokozi katika maisha.Kinyume chake utabaki kuwa mtu wa Mungu.Mpango wa Mungu wa kuwa na familia ulikuwepo kabla ujazaliwa.
Huwezi kuwa nje ya Yesu na bado ukawa sehemu ya familia ya Mungu.Kanisa hatujiungi kama klabu bali kwa kuzaliwa upya.Yoh.3:3.
Biblia inafunua wazi kuwa kunafamilia mbili ya shetani na ya Mungu.Yoh.8:44.Umepewa uamuzi wa kuchugua kuwa familia ya Mungu au ya shetani.

3.UMEUBWA ILI UFANANE NA KRISTO.WARUMI 8:29.

   Kusudi kuu la wokovu ni kutuleta katika  kufanana Kristo.Kwa maana ya Kristo kuonekana katika        maisha yetu.IKor.11:1.
                         
          Ni nini maana ya kufanana na Kristo? I Yoh.2:6. 

  • Kufanana na Kristo ni kumpenda Mungu na kuwapenda watu wengine.Math.22:37;IYoh.4:20-21.Upendo wa Mungu kwa waamini hutuchochea kuwapenda watu wengine.
  • Pendo hudai uaminifu wetu kwa Mungu.Ebr.3:2.

           Tunamwona Yesu akiwa tayari kuyatimiza mapenzi ya Mungu kwa kutoa maisha yake kwa                    ukombozi wetu.Math.26:42.Tunapaswa kuwa waaminifu kutimiza mapenzi yake bila kujari                  ghalama.

  • Pendo la Kristo lilifunuliwa zaidi katika kupenda haki na kuchukia dhambi.Ebr.1:9.

          Kupenda kwake haki na kuchukia uwovu,ndiyo msingi wa Mungu kumpaka mafuta.Kwakufuata           msingi huu upako wa Mungu utafanya kazi juu ya maisha yetu.
          Kristo ni mfano wa kila mwamini hivyo ni lazima tuonyeshe sifa njema, na sio tofauti.Ebr.12:2.

4.UMEUMBWA ILI KUMTUMIKIA MUNGU.WARUMI 12:2.WAEFESO 2:10.

Pasipo nia zetu kufanywa upya,mwamini hawezi kujua wajibu wake katika Kristo.
ni kwa kutafakari neno na Roho mtakatifu.Mimi na wewe kama viungo katika mwili wa Kristo tunao wajibu wakufanya.I Kor.12:14-27.Unapokuwa huna chakufanya katka kanisa shetani atakupa kazi ya kufanya.Mfano tunaweza kuona kwa mfalme Daudi.II Sam.11:1-5.
Ukishindwa kumtumikia Mungu katika maisha yako lazima utamtumikia shetani..

5.UMEUMBWA KWA AJILI YA UTUME.MARKO 16:15-19.

Baada ya tu ya kuwa umeokoka,unalo jukumu la kuvuna roho za watu kwa kuwaleta kwa Kristo.Mith.11:30.

  • Yesu alituita sikumwendea tu bali pia na kwenda kwa wengine kwa ajili yake.Maneno ya Yesu ni maagizo kwa vizazi vyote kama ifuatavyo,

a.Kanisa linapaswa kuenenda ulimwenguni kote na kuhubiri injili kwa watu wote kwa msingi wa Neno    la Mungu.Efe.2:20.
b.Mahubiri yanapaswa kuelekezwa kwenye toba na msamaha.Lk.24:47.
c.Kusudi ni kuwa na wanafunzi wanaofuata maagizo ya Kristo.Yoh.8:31.Mk.1:17.


                     Kwa mafundisho zaidi karibu Beroya Christiani Centre.














Jumatatu, 11 Agosti 2014

KARIBU KATIKA SOMO LA KANUNI YA KUPANDA NA KUVUNA.WAGALATIA 6:7-9.MWANZO 8:22.

Dibaji:Maisha tunayoishi Yesu aliyafanananisha na ukulima.Mkulima anapolima na kupanda nia yake hasa ni kupata mavuno.Kama hunahaja ya kuvuna huna sababu ya kulima na kupata.
Tunahitaji kujua kwa kina namna gani maisha yetu ya wanaweza kuhusika katika kupanda na kuvuna itatusaidia kujihusisha katika kupanda mbegu njema ili kuvuna mavuno mema.
Aina za mbegu:
                      1.Sadaka maalum  2.Maneno 3.Mawazo 4.Matendo.
1.SADAKA MAALUM:2.Kor.9:6-11.Kuna aina tofauti tofauti ya upandaji, kadhalika katika kuvuna.
 a.Kupanda haba,kuvuna haba.Mungu atawabariki wa waamini sawa sawa na utoaji wao.Mith.11:24. Yeye azuiaye  anataka kumiliki kile alichonacho,hataki kuachilia au kutoa,ataelekea kwenye umasikini na ufukara.

 b.Kupanda kwa ukarimu: Nikupanda  mbegu nyingi na kuvuna kwa ukarimu. Kupanda ni kama kutawanya lakini kunakuongezewa. Mith.11:24. Wakati mwingine kupanda ni kama tendo la huzuni,lakini matekeo yake lakini matokeo ya kuvuna ni furaha kubwa.Zab.126:5-6.

 c.Kupanda kwa moyo mkunjufu: Haya huwa ni matokeo ya kujua nitavuna zaidi.Mungu humpenda mtu wa namna hii.2Kor.9:7.

 d.Kusudi la Mungu katika kutubariki: Mungu ndiye huwa anatoa mbegu za kupanda na mkate kwa mkulima.Moja ya sababu ya kukithili kwa uhitaji ni kwa sababu tunakula mbengu amabazo Mungu anataka tuzipande ili azizidishe. Ili tuzidi katika kala tendo njema na kufanyika baraka kwa wahitaji na wa kwaufalme wa Mungu. 2Kor.9:8-11.Mdo.9:36.
Matokeo ya utoaji huu.
-Wahitaji wanapata mahitaji yao
-Watoaji wanabarikiwa 
-Mungu anatukuzwa kwa shukrani.
Kuvuna ni hapa duniani.Mith.11:31.

2.MANENO YA KWINYWA CHAKO:
-Maneno ya kinywa chako huwa ni mbegu ambayo unaponena  ni kama unapanda kwa msingi wa kuvuna.
Mith.18:20-21.Kinywa kina uwezo wa kuzaa kile kisichokuwepo kikawepo.Maana ya mazao ya midomo ni kile kinachozaliwa na midomo.
-Vitu vyote tunavyoviona vimetoka na Neno la Mungu.Ebr.11:3.Ndani ya Uumbaji wote,kuna akili ,wazo,Neno,nguvu,na uhai wa Mungu.

 a.Utu wa ndani:Utu wako wa ndani ni kama Compyutar,chochote unachoingiza ndani ndicho kitakachotoka nje.Math.12:34-37.Kinywa chako kinatawala hatima ya maisha yako-
-Maneno ni kama chombo ya naweza kubeba upendo ,au chuki,mafanikio au umaskini,uzima au mauti.Yana weza kujenga au kubomoa,Hivyo tutavuna.

b.Jinsi ya kubadiri ukili Math.12:34.Nikujaza Neno la Mungu ndani ya moyo  wako.
-Kwa maana  kile unachojaza moyoni mwako ndicho kitakachotawala kinywa chako.Zab.119:11.Kol.3:16.
-Tunahitaji kumwomba Mungu aponye Vinywa vyetu.Zab.19:14.Isa.6:5.Yer.1:9.
-Jenga tabia ya kuisemea mema nafsi  yako siku zote.Zab.103:1-6.1Kor.14:28. Mifano ya watu waliopanda kwa vivywa vyao.-YAKOBO MWANZO 49. NUHU MWANZO 9:24-77.

3.MAWAZO YAKO NI MBEGU:ZAB. 19:14.
    1.Vipo vyanzo vikuu vitatu vya mawazo.
   a.Ulimwengu. Kutokana na unayoyaona na kuyasikia.Maneno huleta picha ya mambo katika akili zetu,na     zikatafakaliwa katika kuleta mawazo.
    b.Mwili.Kutoka na asili ya dhambi.Rum.8:5.
    c.Ibilisi.Kutokana na ulimwengu wa roho,mishale ya moto kwa leo ni mawazo mabaya kutoka kwa              shetani.Efeso.6:16
   2.Chanzo cha matatizo kwa  mtu huanzia ndani ya moyo.
   Math.4:23.Moyo usio safi ni chemchem ya uovu wa kila namna,na mtu hutiwa unajisi kwa hayo.Moyo        huwa kama kiwanda kinachozalisha uovu au wema. Math.15:18-19.Gal.5:19-23.Neno kumtia mtu      unajisi ,humaanisha,kutengwa na uzima,wokovu,na ushirika na Kristo.Zab.66:18.Mawazo ya sio                 matakatifu ya sipo pingwa,huweza kumwongoza mtu kwenye maneno na matendo yasiyo matakatifu.
   3.Jinsi ya kukabiliana na mawazo mabaya.BILLY GRAHAM. Mhubiri wa kimataifa      alisema,huwezi kuzuia ndege kuruka hewani ila unaweza kumzuia kujenga kioto  juu ya kichwa    chako.Akimaanisha huwezi kuzuia mawazo mabaya kuja kwenye ufahamu wako ila unaweza kuyapinga    kukaa kwenye ufahamu wako.
 Jenga tabia ya kupandikiza Neno la Mungu kwenye ufahamu wako,kwa kutafakari.Yosh.1:8.Zab.1:2-            4.Lifikie hatua ya kuwa sehemu ya utu wako wako ndani.
Kwa kutafakari Neno la Mungu,unajenga fikra zako na tabia pamoja na matendo yako katika msingi wa Neno la Mungu.
Kwakusoma Neno la Mungu na kufakari kuna maswali ya kujiuliza binafsi.Je,kuna ahadi hapa kwa ajiri yangu ili nidai? Je,kifungu hiki kinafunua dhambi nayopaswa kuiacha?Je,Mungu anatoa amri nayopaswa kuitii?Je,roho yangu inakubaliana na yale ambayo Roho anasema?Je,kifungu hiki kinaeleza ukweli juu ya Mungu,wokovu na dhambi duniani au utii wangu binafsi  na julishwa na Roho binafsi?

4.MATENDO YAKO NI MBEGU:MATH.7:12.
Kanuni ya kimsingi juu ya mafundisho ya kuhusu maadili.Inafundishwa kwa maneno  ya MATH.7:12.Maneno haya yanajumuisha mapenzi ya Mungu yaliyofunuliawa kupitia sheria na manabii yaani agano la kale lote.Math.22:37-40.Kauli hiyo inasisitiza umuhimu wa watu na mahusiano.
Hatupaswi kuepuka tu kuwadhulumu watu,lakini pia kuchukua hatua ya kuwasaidia wakati wa shida.Chochote unachopanda utakuwa wa kwanza kupata mavuno.2Tim.2:6.
a.Kipimo.Lk.6:37-38,Mith.22:8.Kipimo kiwe cha wema au uovu utakachompimia mtu mwingine ndicho na wewe utakachopimiwa.Kabla ya kufikiri kuwasaitia wengine kwanza tuchunguze maisha yetu kwanza.Wimbo.1:6,Lk.6:41-42.Usiwe mlinzi wa mashamba ya wengine lako ukasahau.
b.Mifano ya ki-Biblia.Kifo cha Naboth.1Fal.21:1-28.Kilikuwa cha hila baada ya kukataa kumuuzia shamba Mfalme Ahabu.Mkewe Ahabu akaanda mashitaka ya uongo dhidi yake akamuuwa yeye na watoto wake.mst.7-15.
Ujumbe wa Bwana kwa Ahabu mst.17-22.Matoke yake. 22:37-38.Kifo cha Yezeberli.11Falm.9:32-37.Vifo vya watoto wa Ahabu.IIFalm.10:6-10.
-Yonathani.
Wakati Mfalme Sauli alipotaka kumuuwa Daudi,Yonathani hakuwa tayari kwa hilo.Yeye alikuwa upande wa Daudi,mbegu aliyopanda kwa Daudi alikuja kuvuna mwanaye.IISam.9:1-8.
c.Ukumbusho mbele za Mungu.Matendo na maneno na sadaka huwa vinahifadhiwa katika kumbukumbu ya Mungu.
-Matendo.
Matendo mema au mabaya.Uf.14:13.20:11-15.
-Maneno.
Math.12:36-37.
-Sadaka na sala.Mdo.10:1-4.
Tusiache kutenda mema hayo ndiyo maisha ya Kikristo.Efe.2:10.Gal.6:9.

             KARIBU BEROYA CHRISTIAN CENTER KWA MAFUNDISHO ZAIDI.